25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

SERIKALI HUKAGUA MADUKA YA FEDHA

NA RAMADHAN HASSAN, DODOMA

NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango,Dk. Ashatu Kijaji amesema Seriali imekuwa ikikagua maduka ya kubadilishia fedha siku hadi siku ili kujiepusha na usafirishaji fedha haramu.

Pia amesema miamala yote ya maduka hayo, ipo chini ya usimamizi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kupitia Mamlaka ya Mapato (TRA).

Hayo yalielezwa jana bungeni na Waziri Dk.Kijaji, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Igunga, Dalaly Kafumu (CCM),  aliyetaka kujua ni kwanini Tanzania imeendelea kutumia Dola za Marekani katika kununua hivyo ni vyema, ikatumia utaratibu wa nchi zingine ambazo zimeachana na matumizi ya dola na zinatumia fedha zao.

Dk. Kafumu alihoji: ‘’ Ni lini serikali itakagua maduka ya fedha kwa kuwa kuna  taarifa za kiuchunguzi  zinaonesha wanatumika kusafirisha fedha haramu?’’

Akijibu swali hilo, Dk. Kijaji alisema Serikali haijalala, BOT kwa kushirikiana na TRA, zinakagua na sasa miamala yote ya maduka ya kubadilishia fedha  yapo chini ya  usimamizi wa serikali.

Alisema BoT kupitia TRA, wanaendelea kuimarisha mifumo ili kuhakikisha fedha  na uchumi unakuwa salama.

Alisema sheria ya Benki Kuu ya mwaka 2006, inasema fedha halali kutumika ndani ya Tanzania ni shilingi, lakini pia katika sheria ya usimamizi wa fedha ya mwaka 1992 inaruhusu mtu yeyote kupokea.

Alisema Serikali imedhamiria kukuza uchumi na kuwa na fedha za kigeni kwahiyo nchi nyingine hufuata utaratibu kutokana na mazingira ya nchi yao.

“Kwa nchi yetu, hatujaona athari kubwa ya kuruhusu wageni kutumia fedha hizo ndani ya uchumi wetu,”alisema Dk. Kijaji

Katika swali la msingi, Dk. Kafumu alihoji: ‘’Ni kwanini serikali isidhibiti matumizi holela ya dola nchini ili kupunguza utakatishaji wa fedha na kuimarisha ukuaji wa uchumi kama zinazovyofanya nchi nyingi duniani?’’

Akijibu, Dk. Kijaji, alisema katika kudhibiti matumizi holela ya fedha hizo, BOT kwa kushirikiana na TRA imeongeza usimamizi katika maduka hayo ambapo kila muamala wa fedha za kigeni unaofanywa zinapaswa kuoneshwa.

“Hatua zimechukuliwa pia kuhakikisha  miamala ya fedha ya kigeni inayofanywa na benki ni ile inayohusu shughuli za kiuchumi tu ili kulinda thamani ya shilingi,”alisema Naibu Waziri huyo

‘’Mkazi yeyote, asilazimishwe kulipia  bidhaa au huduma yoyote hapa nchini kwa fedha za kigeni’’alisema Dk Kijaj

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles