29.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 20, 2024

Contact us: [email protected]

Wakazi Mikocheni wamshukuru Rais Samia

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Wakazi wa Mikocheni jijini Dar es salaam wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa kumteua Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa ambaye amewezesha kuvunjwa kwa maendelezo ya kudumu katika eneo la wazi.

Wakazi hao ambao ni wastaafu wa Kampuni ya Tanzania Karatasi wanaoishi katika maghorofa ya Mikocheni kwa Warioba wametoa shukurani na pongezi za dhati kwa Waziri Silaa leo Desemba 17, 2023 kwa kufanikisha kuondolewa kwa makazi hayo ambayo yalikuwa ni kero kwao kwa muda mrefu.

Itakumbukwa, Novemba 25, 2023 Waziri Silaa alifika eneo hilo na kuelekeza kuondolewa kwa maendelezo hayo ya kudumu ndani ya wiki mbili kwakuwa yamewekwa katika eneo la wazi kwa matumizi ya hifadhi ya barabara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles