26.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

Watanzania waishio nje ya nchi kupewa hadhi maalum

Na Esther Mnyika,Mtanzania Digital

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba, amesema kuanzia mwaka 2024, watanzania wenye uraia nchi nyingine watapewa hadhi maalum ili kushiriki katika maendeleo ya nchi.

Makamba amesema Desemba 17, jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari wakati akieleza mafanikio ya ziara za Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na tathimini ya diplomasia ya Tanzania kikazi.

Amesema katika kuhakikisha hilo linafanyika wamefanya mabadikiliko kifungu cha Sheria ya uhamiaji kinachohusu suala la hadhi maalum katika bunge lijalo.

“Tutangaza hadhi maalumu na stahili mahususi kwa watanzania wanaoishi nje wenye asili ya Tanzania ambao wana uraia wa nchi nyingine kuanza kushiriki kikamilifu katika mchakato wa maendeleo ya nchi yao,”amesema Makamba.

Amesema hadhi maalumu itaanza kutumika mwakani ambapo kupitia hadhi hiyo ya watanzania wataanza kushiriki kikamilifu katika mchakato wa maendeleo ya Tanzania, pia na ustawi wao binafsi ambao unawaunganisha wao na nchi yao.

Makamba ameleza mambo makubwa matano waliyofanya mwaka huu ni pamoja na kukuza biashara na uwekezaji na kukuza kiwango cha utalii nchini na kutafuta fedha.
Amesema pia kuongeza ushawishi katika masuala mtambuka yanayohitaji ushirikiano wa kimataifa, kuimarisha ujirani mwema ushirikiano wa kikundi pamoja usalama, amani na siasa na kuimarisha uhusiano kati ya nchi yetu duniani na taasisi mbalimbali.

Aidha amesema kupitia ziara za Rais Dk Samia mwaka uliopita uwekezaji umekua kwa asilimia kubwa, ajira na kipato kimeongezeka hivyo ni mafanikio makubwa sana.
” Mwaka ujao ni kuendeleza haya tuliofanya ikiwemo kukamilisha na kupitia sera mpya ya mambo ya nje kufungua balozi mpya, “amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles