29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, April 28, 2024

Contact us: [email protected]

Wakazi Dar watakiwa kuchangamkia mkutano wa AGRF

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amewataka wananchi kutumia fursa zitakazopatikana na mkutano mkuu wa jukwaa la mifumo ya chakula Afrika AGRF ili kuboresha shughuli za kilimo

Akizungumza Septemba 1, jiji Dar es Chalamila amesema mkutano huounaotarajiwa kuwa kesho Septemba 5, 2023, amesema utaleta matokeo muhimu katika uendelezwaji wa mfumo wa chakula Afrika, ukuzaji wa sekta ya utalii, biashara na uwekezaji na kukuza teknolojia mpya.

“Jukwaa la mfumo wa chakula la Afrika(AGRF) ni jukwaa kuu la kilimo linalowakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo ili kujadili na kuchukua hatua za kiutendaji katika kuboresha upatikanaji na usalama wa chakula na lishe kwa ujumla,”amesema Chalamila.

Amesema mkutano huo utawakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo wazalishaji, wawekezaji na wafanyabiashara.

Amesema wakazi wa Dar es Salaam wanapaswa kuchangamkia fursa zitakazotokana mkutano huo kwa lengo la kuongeza uzoefu na kujifunza teknolojia za kisasa ili kutimiza malengo ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ya kulisha dunia.

Aidha, Chalamila amewataka wakazi hao kudumisha usalama, ukarimu na usafi ili kuweka taswira ya nchi vizuri.

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Mikutano ya Kimataifa Julius Nyerere (JNICC), Ephrahim Mafuru amesema serikali inatatarajia kupokea wageni zaidi 3,000 wa masuala ya kilimo jumla ya Sh bilioni 12.5 zimetolewa kwa ajili ya maandalizi ya mkutano (AGRF).

Amesema JNICC wamejipanga kuwahudumia wageni hao kwa kutenga jumla ya kumbi 27 ambazo zote maandalizi yake yamekamilika.

“Mchango wa kituo katika mnyororo wa thamani hivyo Serikali kwa kushirikiana na AGRF imejipanga kwa bajeti ya bilioni 12.500 na fedha hizo ni maandalizi ya mkutano ambazo zitaingia katika mnyororo wa thamani wa maandalizi na gharama za kuuendesha mkutano huo,” amesema Mafuru.

Aidha, ameongeza kuwa zaidi ya vyumba 2,600 vya hoteli vimeandaliwa kwa ajili ya wageni hao hivyo amewaomba Watanzania kuwakarimu wageni hao kwani mchango wao ni mkubwa kwa taifa.

Hata hivyo, Mafuru amewataka wajasiriamali watakaopata nafasi ya kushiriki mkutano huo watumie fursa hiyo kukutana na wajasiriamali kutoka nje ya nchi ili kubadilishana uzoefu.

Mkutano huo unatarajia kufanyika nchini kuanzia Septemba 05 hadi 08, mwaka huu katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam na unatarajiwa kufunguliwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles