32.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

Wahuni wampiga Jaji Warioba Dar

makonda vs wariobaFredy Azzah na Shabani Matutu, Dar es Salaam

MDAHALO wa kujadili Katiba inayopendekezwa ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere, jana ulivunjika baada ya kutokea vurugu ambako Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, alipigwa vibao shingoni na watu wanaodaiwa kuwa wanachama wa CCM.

Hali hiyo ilijitokeza kwenye Hoteli ya Blue Pearl iliyopo Ubungo   Dar es Salaam, baada ya kuvunjika  mdahalo huo uliokuwa umehudhuriwa na mamia ya watu, wengi wao wakiwa  vijana.

Baada ya vurugu hizo, waandaji waliamua kuwatoa nje ya ukumbi  wasemaji wa mdahalo huo akiwamo Warioba, Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku, Profesa Palamagamba Kabudi na Profesa Mwesiga Baregu.

Wengine waliokuwa wazungumze kwenye mdahalo huo ni Humphrey Polepole   na Rais wa Chama cha Wanasheria Zanzibar, Awadhi Said, ambao wote walikuwa wajumbe wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Warioba, aliyewahi kushika wadhifa wa Waziri Mkuu na  Makamu wa Rais,   alipigwa vibao viwili shingoni  alipofika kwenye mlango kuu wa kutoka ukumbini ambako kulikuwa na msongamano mkubwa wa watu.  Wakati huo, Warioba na viongozi wenzake walikuwa wakitolewa nje ya ukumbi huo.

Hatua hiyo ilifanya mlinzi wake na baadhi ya watu waliokuwa wakimtoa kiongozi huyo waongeze mwendo na kumkimbiza kiongozi huyo wa taifa kwenye chumba maalumu cha wageni wa heshima (VIP lounge), kilichoko ndani ya hoteli hiyo.

Wakati Warioba akipigwa vibao, miongoni mwa  watu waliokuwa karibu nyuna yake ni Katibu wa Uhamasishaji wa UVCCM, Paul Makonda.

Kwa sababu hiyo,  baadhi ya vijana walichangia kumpiga  kada huyo wa UVCCM aliyekuwa amevalia shati jeupe, huku wakimzuia   kuingia kwenye chumba cha VIP ambako    Jaji Warioba alikuwa amepelekwa.

Kufanikiwa kwa vijana hao kumzuia Makonda kuingia kwenye chumba hicho, kulitoa fursa ya kuendelea kupigwa hadi  alipoponyoka na kukimbilia katika  ofisi moja katika  jengo hilo   na kujifungia.

Baada ya kujificha katika chumba hicho, vijana hao waliitana na kuhamasishana ili wavunje mlango huo na kumtoa Makonda.

Hata hivyo baada kufanikiwa kuvunja mlango huo, vijana hao hawakumuona Makonda hadi walinzi wa hoteli hiyo na askari kanzu walipofika hapo na kuwafukuza.

Vurugu zilivyoanza

Vurugu katika mdahalo huo zilianza muda mfupi kabla ya Jaji Warioba aliyekuwa msemaji wa kwanza, kumaliza hotuba yake.

Baada ya kumaliza kuichambua Katiba inayopendekezwa, Jaji Warioba alisema katika kuitetae katiba hiyo, baadhi ya watu wamekuwa wakimtumia Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu  Nyerere kuunga mkono hoja zao.

“Tunatumia jina la Mwalimu ili kuunga mkono hoja zetu wakati mwingine ninajiuliza hivi tunatumia Mwalimu yuleyule ama…

“Mwalimu amekufa akisema hajaona hata sehemu ya kutia koma katika Azimio la Arusha, kuna watu waliwahi kumletea Mwalimu barua wakimwambia afungue akaunti nje ya nchi ndiyo fedha zake zitakuwa salama… Mwalimu siyo tu   alikataa lakini alitangaza kila kitu hadharani.

“Leo Mwalimu angekuwapo angekubali  watu wafungue akaunti nje ya nchi, angekubali watu wapewe zawadi wakae nazo… nikasema huyo wao siyo Mwalimu, Mwalimu alikuwa ni mtu mwenye uwezo wa kufanya uamuzi mgumu hata unaomhusu yeye,” alisema Warioba.

Vijana na mabango

Baada ya maneno hayo, baadhi ya vijana takriban 20, walisimama na kunyanyua juu mabango yaliyokuwa na ujumbe mbalimbali wa kumtukana Jaji Warioba na mengine yakisifu Katiba inayopendekezwa.

Kitendo hicho kilifanya  baadhi ya watu kujaribu kuwakalisha chini huku wengine wakichana mabango hayo hali iliyozusha  vurugu.

Wakati wote huo  Jaji Warioba alikuwa amesimama akijaribu kuwasihi watu hao kukaa chini, lakini hali hiyo ilionekana kutozaa matunda.

Baada ya muda vijana hao walijitenga pembeni karibu  na jukwaa kuu huku wakiwa na mabango yao, wakiimba nyimbo mbalimbali za CCM.

Hali hiyo ilisababisha  baadhi ya watu watoke  ukumbini  huku  wengine wakiwa wanarudi kuketi kwenye viti vyao.

Wakati vurugu hizo zikiendelea, Profesa Kabudi na Butiku kwa nyakati tofauti, walionekana wakimtaka Makonda kuwatuliza vijana hao wa CCM ambao alidaiwa yeye yeye ndiye aliwaingiza katika  ukumbi huo.

Wakati viongozi wakimtaka Makonda kufanya hayo, vijana wengine walionekana kumvuta Makonda wakitaka kumpiga hali iliyomlazima kumtumia kama kinga, Amon Mpanju, ambaye alikuwa Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba akiwakilisha kundi la walemavu.

Hali  iliendelea hivyo hadi baadhi ya vijana waliokuwa wamekaa  walipohamasishana na kuwapiga wale waliokuwa na mabango, kwa kutumia  viti hali iliyofanya wakimbie na kutoka nje ya ukumbi huo.

Baada ya vijana hao kutoka nje, hali iliwageukia Makonda na Mpanju ambao baada ya kuona hali imekuwa tete, walikimbilia kwenye jukwaa kuu na kukaa karibu na Jaji Warioba.

Huku hali ikiwa bado ya taharuki, viongozi hao (Warioba na wenzak)  waliamua kutoka nje ya ukumbi na ndipo zahama ya kupigwa vibao kwa Jaji Warioba ilipojitokeza.

- Advertisement -

Related Articles

14 COMMENTS

  1. makonda unatafuta nini?,ubunge, uwaziri ama umeadiwa nini na hao wanaokutuma.kijana mdogo msomi unatumiwa kiraisi hivyo kufanya mambo kifezuli. hivi nikuulize makonda unafikiri unavyofanya vitakupa sifa ama utachukua heshima ya nyerere ikawa yako ubafikiri unayofanya yatakupa heshima NDANI ya choma chako unajidanganya .sisi wananchi ndio wenye maamuzi ya mwisho na hiyo katiba sio wewe na utumwa wako WA mawazo. Mimi sikutofautishi na wasanii WA bongo wanaotumia skendo kujipatia jina , unapotea ndugu Yangu na nikwambie laana ulioipata baada ya kumpiga chupa jaji warioba itakutafuna na itafuta ndoto yako ya kuwa mbunge katika nchi Hii.

  2. Mr makondeeee naona umeanzisha genge la judo unatoa kichapo kwa wakubwa zako. kale kabachelor chako umekaweka mfukoni.umeamua kuitimu mafunzo yako ya ukomandoo kwa kumchapa chupa walioba. umepewa shilingi ngapi au cheo kipi tutegemee kutoka kwako.ongera baba naona huu mwanzo tu habari yenyewe April etiii.wangekuwa chadema mngeongeaaaa Leo tumewaona. soma alama za nyakati baba membe,sitta ,nape hawamuwezi luwasa,pinda ,ama januari.jitaiditaidi ubunge labda utapata WA kuongoza familia yako.

  3. Kwa kusema kweli hali inatisha kama viongozi wetu wanaoelekeza ni wapi pako sawa na wapi turekebishe wanafanyiwa mizengwe,ufike muda hicho chama kinachowatuma na kuwalea iwe basi,kinatia nchi aibu kubwa mno,karne ya kujifunza kusoma na kuandika imekwisha.

  4. Warioba na wenzako kazi yenu iliisha hakuna aliyeingilia kati.Mbona ninyi hamfuati utaratibu huo wa kiistarabu.Watanzania sio mbumbu unavyodhania wewe.Maana ni dhahiri umeungana na UKAWA ni vyema ukajitangaza hivyo.Taasisi ya Mwalimu Nyerere inatumika visivyo lakini yote yanajulukana.

  5. Jamani waandishi wa habari tusaidien kutupa ukweli kitu kinachoendelea hapa tz maana sisiweingine habari tunazipata kwa kutegemea nyie.

  6. Kimsingi kifo cha maji lazima utapetape, kipindi wana wa Israel wanavuka bahari ya Shamu majeshi ya Farao yaliendelea kuwafuata wana wa Israel, majeshi ya Farao yalikuwa na macho lakini hayakuona wana wa Israel walikuwa wakiongozwa na Mungu hata maji yakatengeneza barabara katikati, kilicho tokea jeshi lote la Farau, magari na farasi viliangamia baada ya wana wa Israel kuvuka bahari. ndivyo watakavyo angamia wapinga katiba ya kweli, Naamini kuelekea kupata katiba mpya ni sawa na safari ya wana wa Israel lazima tutafika na itapatikana tu na wapinzani wa katiba ya kweli watashindwa, kwani Mungu ataisimamia. Sema Amina

  7. Kila jambo linamwisho hiyo ni rahana kubwa sana kupiga mzee wa heshima,tumefikia wakati tumewazalau mpaka wazee kwa maama nyingine taifa halina maadili.Ila siku zote Mungu anapoamua kumuondoa mtu uwa anamfanya kama kipofu na hata awa watawala wamefanywa vipofu kila jambo wanalofanya wakizani ni zuri linaonekana kinyume katika jamii.Mzee warioba nakutia moya endelea mbele Tutafunga na kuomba ipo cku nchi hii itabadirika .Vijana pia tuamke nchi hii inatuhusu sana bado tunasiku nyingi za kuishi tumelala mpaka wazee ndiyo wanakuwa na uchungu mpaka kuzalilishwa namna hii.

  8. Paul Makonda ajisikie aibu na atumie akili asiwe mjinga kiasi hiko. Vijana wa Tanzania kwanini tunakuwa wagumu wa kufaham ni bora Alshabab waje watutie adabu huenda tukaelewa umuhimu wa amani na ulizi imara wa Nchi na wananchi, Hivi kwani ungemsikiliza akasema anayoamini na wewe ukamuuliza kwanini anaamini hivyo akakupa hoja ukapima kwa akili yako sio lazima tulazimishane kukubaliana. Inatia Kinyaa Tanzania. najuta kuzaliwa Tanganyika

  9. Hapa tatizo watawala wetu hawajawa tayari kupokea mabadiriko kutoka kwa mtu asiyekuwa ndani ya mfumo kama wanavyofikilia wa lakini nawashauli. “unapoitwa kiongozi kubali ushauri na ushauri sio lazima utegemee kupata ushauri unaokupendeza wewe na maana ya ushauri ni kwamba unapewa usichokijuwa ili ukifanyie kazi wala sio kumzuia anayekushauri” jamani Dunia imefikia hapa hata usipkubali mabadiliko siku moja utayaona bila wewe kuyakubali ndipo utajiona ovyo kweli. tunaomba msituongoze kwa mazoea.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles