Wahujumu miundombinu ya umeme wakamatwa

Na MWANDISHI WETU

-DAR ES SALAAM

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), limeendesha msako mkali wa kuwasaka watu wanaohujumu miundombinu ya umeme.

Katika msako huo watu tisa wamekamatwa wakituhumiwa kuhusika na wizi wa mafuta ya transfoma huku wakiwa na  madumu 68 ya lita 20 ambayo nayo yalikamatwa.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, alisema watuhumiwa hao walikamatwa wakiuza mafuta hayo maalumu kwa ajili ya kulainisha vifaa vya magari.

Alisema uchunguzi wa awali umebaini mafuta hayo wamekuwa wakichanganya na vimiminika vingine na kutengeneza Engine Oil ambayo huiuza kwa watumiaji wa vyombo vya moto kama magari.

“Aprili 29, 2019, watuhumiwa wawili tuliwakamata wakiwa na vibati vya transfoma ambapo walieleza kuwa huvitumia vibati hivyo kutengeneza mashine za kuchomelea,” alisema Mambosasa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here