26.7 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Mahakama yawaweka chini ya uangalizi washtakiwa

Na AVELINE KITOMARY

-DAR ES SALAAM

MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala Dar es Salaam imewawekaka chini ya ungalizi kwa mwaka mmoja watu wawili kwa kuhusishwa na makosa ya jinai yanayosababisha uvunjifu wa amani katika jamii.

Waliowekwa chini ya uangalizi ni Omary Abdallah na David Joseph Wakazi wa Dar es Salaam.

Uamuzi  huo ulikuja mara baada ya Ofisa wa Polisi Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam, Anaeli Mbise kuandika barua iliyoomba amri ya mahakama ya kuwaweka watu hao chini ya uangalizi.

Akisoma ombi hilo mbele ya Hakimu Adelf Sachore, Wakili wa Serikali Grace Mwanga,  alisema Jeshi la Polisi limetoa ombi hilo kutokana na watu hao kujihusisha na makosa ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na wizi jambo ambalo kumekuwa likilalamikiwa na jamii iliyowazunguka.

Watuhumiwa hao wote wawili walikubali kuwekwa chini ya uangalizi, hata hivyo mahakama imetoa amri kwa watuhumiwa hao kuripoti Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam kila mwezi kuanzia  Juni 1 mwaka huu hadi Juni 1, 2020 kwa wakati wote watakapokuwa chini ya uangalizi.

Hakimu Sachore alisema dhamana iko wazi kwa watuhumiwa kuwa na wadhamini wawili na mmoja awe anatoka katika taasisi inayotambulika ambao watatoa bondi ya Sh milioni moja kwa kila mmoja.

Hata hivyo watuhumiwa walishindwa kukidhi masharti ya dhamana na kupelekwa rumande mpaka Mei 14, mwaka huu kwa ajili ya kutimiza dhamana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles