Waganga wahimizwa kuwafichua wahalifu

0
1691

mganga

Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Tiba za Asili Tanzania (Shivyatiata),  Abdulrahman Lutenga, amewataka waganga wote nchini kuwafichua wenzao waonajihusisha na vitendo vya upigaji ramli chonganishi   na kuwatakasa majambazi.

Lutenga alikuwa akizungumza na waganga wa tiba asilia  wilayani Maswa jana.

Alisema    ili kutatua changamoto zilizopo ni vema kukawa na utaratibu wa kuchunguzana na kutambuana  katika kazi zao.

Bila   kuwafichua waganga wanaosaidia uhalifu, wote wanaweza kuhesabiwa kuwa wahalifu, alisema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here