27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Watoto 197 wafanyiwa upasuaji vichwa vikubwa, migongo wazi

VICHWA

Zaidi ya watoto 197 wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi wamefanyiwa upasuaji kwa ushirikiano wa kampuni ya GSM na Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI).

Kaimu Mkurugenzi wa taasisi hiyo Dk.Othman Kiloloma, alisema watoto waliofanyiwa upasuaji ni awamu ya pili ya kampeni ya kusaidia watoto wenye vichwa vikubwa inayofadhiliwa na GSM na tayari wameshafanyia upasuaji watoto kwa mikoa tisa.

Alisema mbali na kufanya upasuaji waliweza kuwafanyia vipimo  watoto 800 wenye matatizo mbali mbali wakiwemo wa vichwa vikubwa.

Dk. Kiloloma alisema taasisi yao inatarajia kufanya tena upasuaji wa watoto wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi kwa awamu ya tatu ambapo wanatarajia kutembelea mikoa mitano.

Alisisitiza kuwa mtoto mwenye kichwa kikubwa na mgongo wazi kama atawahishwa hospitali mapema na kuonwa na madaktari upo uwezekano mkubwa wa kuokoa maisha yake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles