25.2 C
Dar es Salaam
Monday, December 2, 2024

Contact us: [email protected]

WADAU AZAKI WAPIGWA MSASA

Mwenyekiti wa Shirika lisilo la Serikali la Utetezi wa Haki za Binadamu, (THRDC), Onesmo Olengurumwa
Mwenyekiti wa Shirika lisilo la Serikali la Utetezi wa Haki za Binadamu, (THRDC), Onesmo Olengurumwa

NA HARRIETH MANDARI-DAR ES SALAAM

MWANASHERIA Horace Adjolohoun amewataka wadau wa Asasi za Kiraia  (Azaki) kuhakikisha wanapata elimu ya kutosha juu ya taratibu za kisheria zitakazowasaidia kutoa msaada.

Kauli hiyo aliitoa Dar es Salaam jana, alipofungua mafunzo ya haki za binadamu kwa Azaki kuhusu kutumia njia mbalimbali za kikanda kutetea haki za binadamu.

“Nchi nyingi za Bara la Afrika zina  vyombo vingi vya kutetea haki za binadamu na pia wameingia mikataba mingi ya aina hiyo, lakini haifanyiwi kazi kutokana na wahusika kukosa uelewa juu ya taratibu za kufuata wakati wa kutafuta haki,” alisema Horace, ambaye ni mwanasheria wa kimataifa.

Alisema wakati umefika sasa kwao kuacha kuyaweka makubaliano hayo katika makaratasi tu na badala yake kuyafanyia kazi na kuhakikisha matatizo yote yanayowakumba wananchi yanayohusu ukiukwaji wa haki za binadamu yanafanyiwa kazi.

Naye Mwenyekiti wa Shirika lisilo la Serikali la Utetezi wa Haki za Binadamu, (THRDC), Onesmo Olengurumwa, alisema ipo haja ya kutoa mafunzo ya mara kwa mara kwa watendaji wa asasi za kiraia, hasa linapokuja suala la ukiukwaji wa haki za binadamu.

Alisema hapa nchini bado watendaji wa Azaki wanakumbwa na changamoto ya kushindwa kupeleka malalamiko yao katika vyombo vya kisheria vya kimataifa, kutokana na kukosa elimu ya taratibu za kufuata.

“Kwa sasa nchini Tanzania zipo asasi 400 ambapo ni sita tu kati ya hizo zinatambulika kimataifa, ambazo hazitoshi kukidhi mahitaji ya jamii,” alisema Onesmo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles