22.3 C
Dar es Salaam
Saturday, July 13, 2024

Contact us: [email protected]

Wachimbaji madini ya viwandani waomba Serikali kuweka mkazo bei elekezi

Na Mwandishi Wetu, Mwanza

Wachimbaji wadogo wa madini  ya viwandani nchini wameiomba serikali kuweka mkazo kwenye utekelezaji wa bei elekezi ili kufanya uchimbaji huo uwe na tija kwa wauzaji na wafanyabiashara kupata faida wanayostahili.

Hayo yameelezwa Mei 8, 2023 na Mwenyekiti wa Kamati ya Madini ya Viwandani ya Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Wadogo wa Madini Tanzania(FEMATA), Alhaji Idd  Leonard Mhina wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu changamoto zinazowakabili katika maonesho ya wiki ya madini inayoendelea kwenye viwanja vya Rock City Mall, Mwanza.

Alhaji Mhina amesema  licha ya serikali kuweka bei elekezi kwenye ununuzi wa madini ya viwandani ikiwamo chuma lakini baadhi ya wawekezaji na wenye viwanda wamekuwa wakiwanyonya Watanzania kwa kutofuata bei hiyo jambo ambalo limesababisha baadhi yao kushindwa kuendelea na shughuli ya uchimbaji madini hayo hivyo kuikosesha mapato serikali.

“Hali hiyo pia inatusababishia tushindwe kuaminika kwenye taasisi za fedha maana tunaandika andiko la kuomba  mkopo kwa bei elekeze  unachukua fedha lakini ukipeleka mzigo kiwandani mwenye kiwanda anakulipa bei anayotaka yeye kwa kisingizio kwamba mzigo hauna ubora,”ameeleza Alhaji Mhina na kuongeza:

“Kwa mfano mimi Mwenyekiti ambaye pia ni Mwenyekiti wa  Femata mkoa wa Tanga pamoja na wenzangu zaidi ya 10 yamenitokea kwenye oda yangu na moja ya kiwanda kikubwa nchini tulikuwa na makubaliano ya kuuza tani 10,000 kwa mwezi yenye thamani ya Sh milioni 470 baada ya kodi, lakini tulipomfikishia mzigo hatukulipwa chochote wakidai mzigo hauna ubora kwahiyo sisi ndiyo tunaingia hasara na mzigo wenyewe hawakurudishii,” amesema.

Mwenyekiti huyo ameiomba serikali kuwasaidia kwa kuweka wanasheria ili wachimbaji hao wapate haki yao, huku akidai wamiliki wengi wa viwanda wameanza kuchimba wenyewe madini ya chuma jambo linalowaathiri wachimbaji wadogo kukosa soko la bidhaa yao.

Mchimbaji mwingine wa madini ya chuma kutoka Mkoa wa Dodoma, Salum Sanga amesema bei elekezi ya serikali ni Sh 60,000 kwa tani moja, mwekezaji akifuata madini machimboni anauziwa Sh 40,000 lakini changamoto iliyopo ni kwamba wakipeleka tani 2000 mwenye kiwanda anakata  tani 1,000 akidai iko sawa na tano zingine 1,000 anadai hazina ubora.

“Ukiomba material anakuwa amekwishayatumia sasa kama hayako sawa kwa nini ayatumie?,” alihoji Sanga na kuongeza:

“Mimi nimefilisika kwa sababu fedha yote imebaki kwenye material ambayo niliambiwa  hayana ubora hivyo mtaji wangu wote ukawa umebaki kwenye huo mzigo material hayo yalikuwa ni tani 2,000 ambayo sawa na Sh milioni 80 hii imefanya niache kuchimba madini chuma kwa miaka minne sasa.

“Ninachoiomba serikali  iwasimamie wenye viwanda kwa sababu wanatumia ujanja kutudhulumu kupitia ubora wa material,”amesema Sanga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles