25.5 C
Dar es Salaam
Saturday, May 18, 2024

Contact us: [email protected]

Askofu Kijanga atunukiwa Udaktari, Dc atoa neno

Na Seif Takaza, Singida

MKUU wa Wilaya ya Iramba mkoani wa Singida, Suleiman Mwenda ampempongeza Mchungaji wa Kanisa la EAGT la mjini Kiomboi Askofu Dk. Robert Kijanga kwa kuliheshimisha kanisa hilo hadi kufikia hatua ya kupata Shahada ya Heshima PHD.

DC Mwenda alitoa pongezi hizo juzi katika hafla ya kumpongeza mchungaji huyo iliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri baada ya kutunukiwa Shahada ya Heshima aliyepatiwa na Chuo cha All Nations Christian Church International University cha nchini Marekani.

Mwenda amesema amemfaham Mchungaji Kijanga baada ya kufika Iramba ambapo alimwomba kuwa Mgeni Rasmi kugawa magodoro kwa Watoto ambao wako katika mazingira magumu.

“Ndugu zangu Askofu Dk. Kijanga anastahili Shahda ya heshima kwani anafanya mengi pamoja na Utumishi wa Mungu ameliheshimisha kanisa lake kwa kufanya mambo mengi katika kuendeleza jamii ambayo yamestahili kupata shahada hiyo.

“Ninayo fahari kubwa katika Wilaya yangu kwa kuwa na Daktari mwingine baada ya Mbunge wetu Dk. Mwigulu Nchemba, hii inanipa faraja na kunipa watu wenye maono ya kuendeleza wilaya hii,” amesema Mwenda.

Aidha, Mwenda alisema kwa kutumia hadhara hiyo anawaomba viongozi wa dini, wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kuhakikisha wanawapa maadili mema watoto wao kwani kwa sasa kuna mmomonyoko mkubwa wa maadili hivyo inawapasa kuwa makini sana ili watoto wasipotee na kufuata maadili yaliyo nje na utamaduni na mila zetu.

Kwa upande wake, Askofu Dk. Kijanga amemshukuru Mkuu wa Wilaya hiyo kwa kukubali kuwa Mgeni Rasmi katika hafla hiyo iliyotukuka akiwa pamoja na mke wake na wachungaji wengine waliofika kumuunga mkono.

“Mheshimiwa Mkuu wa wilaya kwa heshima na taadhima nakushukuru kwa dhati kuja katika hafla hii, Mungu akubariki wewe na familia yako muweze kulitumikia Taifa hili. ninaomba nimpongeze kwa dhati kwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanya katika nchi yetu kwa kuleta usawa kwa taifa lakini pia amekaa na vyama vya siasa na kufanya maridhiano ya kujenga nchi yetu,” amesema Askofu Dk. Kijanga na kuongeza kuwa:

“Mheshimiwa Mkuu wa wilaya nakuomba salamu zangu zimfikie mheshimiwa Rais ya kwamba sisi vingozi wa dini tuko pamoja na tunaahidi kumsaidia na kumuombea yeye na Serikali yake.

“Sisi viongozi wa dini tunakemea vitendo vya ndoa ya jinsia moja, usagaji na unyanyasaji kwani yanaenda kinyume na maandiko matakatifu mfano wa Sodoma na Gomora hatutapenda nchi yetu iharibike,” amesema Askofu huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles