26.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 3, 2022

WABUNGE WAHOJI UNYANYASAJI WA WAVUVI

Ramadhan Hassan, Dodoma

Wabunge wamehoji ni kwanini serikali haiweki utaratibu wa upatikanaji wa nyavu za kuvulia kwa wavuvi na badala yake imekuwa ikiwanyanyasa kwa kutokujua ni aina gani ya vyavu wanatakiwa kutumia wakati wa kuvua.

Mbunge wa Geita, Costantine Kanyasu (CCM), amesema kwa sasa kilio cha wavuvi ni kunyanyaswa na serikali kuhusiana na aina ya nyavu wanazotakiwa kuzitumia.

“Kwa sasa kilio cha wananchi ni unyang’anyi mkubwa unaofanywa na wizara hii, kuna bahati mbaya tunatumia nguvu kubwa lakini majibu ya serikali ni mepesi.

“Kwa sasa hakuna nyavu madukani, wavuvi wameacha kununua nyavu za Tanzania kwa sasa wananunua za Kenya na Uganda, kwanini Waziri anazuia nyavu, unataka watu wavulie nini, siungi mkono hoja waziri atuambie ni kwanini tunateseka,” amesema Kanyasu.

Naye Mbunge wa Ukerewe, Joseph Mkundi (Chadema) alihoji kuhusiana na operesheni Sangara kuwadhulumu wavuvi.

“Uchumi wa taifa unategemea mtu mmoja mmoja na uvuvi unachangia pato la taifa asilimia 2.2 lakini sioni kama kuna umakini katika hili.

“Uvuvi Kanda ya Ziwa ni siasa mfano operesheni Sangara ni uonevu na udhulumati mkubwa, wavuvi wanafanyiwa vitendo vya ajabu kabisa.

“Operesheni Sangara inawanyima uhuru Wavuvi watu wahuni tu wanawachomea nyavu zao,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,573FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles