30.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 25, 2022

MBUNGE CHADEMA ASEMA WIZARA YA MIFUGO NI HEWA

Ramadhan Hassan, Dodoma.

Mbunge wa Serengeti, Marwa Chacha (Chadema) amedai Wizara ya Mifugo na Uvuvi ni Wizara hewa ambapo pia amehoji ni kwanini Serikali imekuwa ikiwanyanyasa wavuvi kwa kuwanyang’anya nyavu zao.

Akichangia bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi bungeni jijini Dodoma leo Mei 17, wizara hiyo ilitengewa fedha za maendeleo Sh bilioni nne lakini hakuna fedha waliyopewa.

“Najiuliza kwanini wameiweka hii wizara peke yake na kuitenganisha na Kilimo au ilikuwa kuwatafutia ‘washkaji’ ulaji, maana yake ni kwamba hamtaki kusikia biashara ya wavuvi nchi hii.

“Ng’ombe 300 wamepigwa mnada ila tembo akila shamba la ekari tano mhusika analipishwa faini ya Sh 100,000 kwa ng’ombe mmoja.

“Wafugaji wetu wanapata shida mtapata hela wapi Ulega (Abdallah, Naibu Waziri wa Kilimo) mwaka uliopita hamkupewa hata 100 afadhali mje hata mimi naweza kuwafadhili,” amesema Marwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
201,896FollowersFollow
553,000SubscribersSubscribe

Latest Articles