24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Wabunge Uingereza waanza mjadala wa kujiondoa EU

LONDON, UINGEREZA

WABUNGE wa Uingereza jana walianza mjadala wa siku tano kuhusu mpango wa Waziri Mkuu Theresa May wa kuiondoa nchi hiyo kutoka Umoja wa Ulaya (EU) maarufu kama Brexit, ambao unakabiliwa na upinzani mkubwa.

Serikali ya Uingereza ilitangaza kwamba wabunge hao watapiga kura Jumanne wiki ijayo kuhusu makubaliano ambayo May aliyafikia na EU huku ikikanusha madai kuwa huenda ikataka mpango huo ucheleweshwe iwapo makubaliano yatakataliwa.

May bado anatafuta hakikisho kutoka EU kuhusu masuala tete ya Brexit yanayohusu Ireland ya Kaskazini, ili kuwashawishi wakosoaji kuunga mkono.

Hakikisho hilo linatarajiwa kuwasilishwa kwa wabunge hao kabla ya kupiga kura, lakini si kabla ya kuanza mjadala jana.

Serikali ya Uingereza awali ilikuwa imejiandaa kujiondoa EU bila makubaliano yoyote, huku ikitarajiwa kujiondoa Machi 29, bila kujali iwapo mpango wa May utakubaliwa au vinginevyo.

May anasisitiza kuwa Uingereza itajiondoa EU ifikapo Machi, lakini kuna mazungumzo yanayoendelea ya kuchelewesha mchakato huo ili kumpa nafasi ya kuhakikisha mpango wake unapitishwa.

Mmoja wa wanadiplomasia wa EU alisema wanaamini iwapo makubaliano ya Brexit yatakataliwa bungeni, May atataka mchakato huo uahirishwe.

Inadaiwa kwamba kwa wiki kadhaa Uingereza imekuwa ikijadili uwezekano huo, lakini Waziri wa Brexit, Stephen Barclay amekanusha ripoti hizo akisema kuna baadhi ya watu katika Umoja wa Ulaya wanaojadili suala hilo, lakini huo si msimamo wa Serikali ya Uingereza.

Wanaounga mkono mpango wa Brexit wana wasiwasi kuwa hakuna mbinu ya Uingereza kujiondoa peke yake, ikimaanisha huenda ikasalia katika umoja huo milele, hivyo kuathiri uwezo wake wa kufikia makubaliano na mataifa mengine duniani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles