WAANDISHI WA REUTERS WAHUKUMIWA MIAKA SABA JELA

0
569

 

RANGON, MYANMAR


Wanahabari wawili wa Shirika la Habari la Reuters walioshtakiwa kwa kukiuka sheria inayohusu siri za dola nchini Myanmar, wamehukumiwa kifungo cha miaka saba jela.

Hukumu hiyo iliyotolewa jana, imesababisha shutuma zaidi, ikiwa ni wiki moja baada ya ripoti ya utafiti ya Umoja wa Mataifa kulishutumu jeshi la Myanmar kwa mauaji ya kimbari.

Waandishi hao, Wa Lone (32) na Kyaw Soe Oo (28), walikuwa wakizuiliwa katika gereza la Yangon tangu walipokamatwa Desemba mwaka jana walipokuwa wakiripoti mauaji dhidi ya jamii ndogo ya Waislamu wa Rohingya.

Walishtakiwa kwa kukiuka sheria ya siri za dola ambayo iliasisiwa na ukoloni wa Kiingereza, na ambayo adhabu yake ni kifungo cha hadi miaka 14 jela.

Kampeni ya jeshi ya safishasafisha katika Mkoa wa Rakhine, ilisababisha Warohingya 700,000 kukimbilia nchi jirani ya Bangladesh na kusimulia visa vya ubakaji, mauaji na nyumba zao kuchomwa moto.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here