30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

MAVUNDE: UCHAGUZI MDOGO HAUATHIRI IDADI YA VITI MAALUMU

|Mwandishi Wetu, Dodoma



Serikali imesema mabadiliko yanayotokea katika uchaguzi mdogo wa ubunge, hayaathiri idadi ya viti maalumu vya chama husika.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Maunde amesema hayo akijibu swali la  Mbunge wa Viti Maalumu, Angelina Malembeka aliyetaka kujua hatima ya wabunge walioingia bungeni kupitia asilia za majimbo yao ya uchaguzi.

“Kwa kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimeongeza idadi ya majimbo, je ni lini wabunge wapya wa CCM kupitia viti maalumu wataingia bungeni?” alihoji Malembeka.

Akijibu swali hilo Mavunde amesema idadi ya wabunge wa Viti Maalumu kwa kila chama inapatikana wakati wa uchaguzi mkuu ambao hufanyika kila baada ya miaka mitano.

“Hata hivyo, serikali imeendelea kupokea maoni na ushauri kuhusu jambo hili, kutokana na hali ilivyo kwa sasa Katiba na Sheria za nchi vitaendelea kuwa msingi mkuu wa ufafanuzi na mgawanyo wa wabunge wa viti maalumu bungeni,” amesema Mavunde.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles