25.2 C
Dar es Salaam
Sunday, August 14, 2022

Viziwi walia na mitaala ya elimu

mwkt

JOHANES RESPICHIUS, DAR ES SALAAM

CHAMA cha Viziwi Tanzania (CHAVITA), kimeilalamikia idara ya elimu nchini kwa kutokuwa na mitaala maalumu ya kuwafundishia wanafunzi wenye ulemavu huo  shuleni.

Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa CHAVITA, Nidrosy Mlawa, wakati alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya wiki ya viziwi Duniani ambayo yatafanyika kitaifa jijini Tanga.

Alisema licha ya Dira ya maendeleo kuridhia kuwepo kwa lugha ya alama lakini inaonekana kwenye makablasha bila kufanyiwa kazi.

“Viziwi hawana mitaala maalum ya kufundishia unakuta mitaala tuliyonayo ni ya jumla hivyo wanaofundishwa mwanafunzi asiyekuwa na tatizo la usikivu ndio ule ule unaotumika kwa kiziwi.

“Kuna haja ya wataalamu wa masuala ya kuandaa mitaala kutushirikisha sisi viziwi wenyewe kuchambua kwa kina ili mwishowe tutengeneze mitaala ambayo ni maalumu kuwafundisha viziwi,” alisema Mlawa.

Alisema ukosefu wa huduma ya wakalimani katika maeneo ya matukio muhimu yanawafanya viziwi kuonekana hawawezi licha ya baadhi kuwa na taaluma mbalimbali.

Aidha alisema changamoto nyingine ambayo ambayo imekuwa ikiwakabili viziwi ni kukosa chuo maalumu kinachofundisha walimu wa lugha ya alama badala yake asasi zao ndizo zimekuwa zikifanya kazi ya kuwafundisha na kutoa vyeti licha ya vyeti hivyo kutotambuliwa na Serikali.

“Tulipendekeza kwamba Chuo cha Katangi Arusha kiwe na mkalimani ambaye atakuwepo muda wote lakini hakuna utekelezaji wowote kutoka Idara ya elimu kwa niaba ya Serikali,” alisema Mlawa.

Alisema CHAVITA kina mpango wa kuhakikisha lugha ya alama inafundishwa kuanzia shule za misingi ili kila mmoja awe na uwezo wa kuwasiliana na kiziwi kwa urahisi tofauti na ilivyo sasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,695FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles