31.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

Vituo vya kutibu dengue Tanga vyafikia 11

Amina Omari -Tanga

MKOA wa Tanga umesogeza huduma ya upimaji wa ugonjwa wa dengue kutoka vituo vitatu hadi kufikia 11 kwa lengo la kuongeza kasi ya upimaji ugonjwa huo.

Hayo yamesemwa juzi na mratibu wa magonjwa yanayopewa kipaumbele mkoani hapa, Josephine Kapinga wakati akitoa taarifa ya udhibiti wa ugonjwa huo kwa waratibu wa afya na mazingira.

Kapinga alisema kutokana na kuongezeka vituo hivyo, kumesaidia kupunguza msongamano wa wagonjwa ambao walikuwa wanategemea vituo vichache.

Alisema wizara husika imewasaidia vifaa vya kupima bure ambavyo vimesambazwa vituo vya afya vya Serikali na kusababisha kasi ya upimaji kuwa kubwa.

“Kwa mfano, Julai hadi kufikia jana, kesi za wagonjwa wa dengue zimepungua hadi kufikia mgonjwa mmoja pekee, inatokana na elimu ya usafi inayoendelea kutolewa kwa wananchi,” alisema Kapinga.

Alisema tangu Januari hadi Juni, mwaka huu, wagonjwa waliopimwa ni 967, waliogundulika na ugonjwa huo ni 303, huku kifo kikiwa ni kimoja, Wagonjwa wote walitoka Wilaya ya Tanga.

Kapinga alisema tayari hatua mbalimbali za kudhibiti ugonjwa huo zimeshachukuliwa, ikiwamo upuliziaji wa dawa katika mabasi ya abiria, mifereji  na makazi ya watu.

“Tayari Tanga Jiji wamefanikiwa kutoa elimu ya kujikinga na ugonjwa huo kwa walimu 150 wa shule za msingi ili waweze kutoa elimu,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles