26.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 27, 2023

Contact us: [email protected]

Wajasiriamali watakiwa kurejesha fedha za mikopo

Mary Mwita -Monduli 

 MAKUNDI maalumu ya wajasiriamali ya wanawake, vijana na walemavu ambayo yamepatiwa mikopo na Halmashauri ya Wilaya ya Monduli mkoani Arusha, wametakiwa kuirejesha kwa wakati kama walivyoelekezwa kwa mujibu wa sheria.

Hayo yalisemwa jana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli, Isack Joseph wakati akikabidhi mikopo yenye thamani ya Sh milioni 131 kwa vikundi 41 vya kinamama, vijana na walemavu.

Joseph alisisitiza urejeshwaji wa mikopo hiyo kwani si zawadi.

Alisema hatua ya kukabidhiwa mikopo hiyo inatokana na mazingira mazuri na rafiki waliyowekewa na Rais Dk. John Magufuli ikiwa ni pamoja na kuagiza kutolewa kwa vitambulisho vya wajasiriamali wadogo.

Ofisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya, Faudhia Omari, ambaye alitoa taarifa kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri, Rose Mhina, alisema kuwa wanakabiliwa na changamoto ya baadhi ya wakopaji kubadilisha miradi na kuchelewa kurejesha mikopo.

Alisema kuchelewa kurejeshwa kwa mikopo kunasababisha baadhi ya waombaji kutoka katika vikundi kuchelewa kupata na kutaka watu wanaokopa kurejesha kwa wakati.

Kwa upande wao, baadhi ya wanufaika walisema kuwa Serikali imewakomboa na mikopo isiyokuwa na riba na kuahidi watarejesha kwa wakati ili wengine waweze kukopa kwa wakati.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,206FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles