23.2 C
Dar es Salaam
Friday, May 10, 2024

Contact us: [email protected]

VITA LIGI YA MABINGWA ULAYA KUENDELEA LEO

DORTMUND, UJERUMANI

KIVUMBI cha michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kinatarajia kuendelea leo kwenye viwanja mbalimbali huku mchezo unaotarajiwa kuvuta hisia za mashabiki wengi na wadau wa soka ni kati ya Borussia Dortmund ambao watakuwa kwenye uwanja wa nyumbani na kuwakaribisha wapinzani wao, Real Madrid.

Ni mara ya pili kwa timu hizo kukutana hatua ya makundi kwa misimu miwili mfululizo, msimu uliopita zilitoka kwa kufungana mabao 2-2, lakini Dortmund wamekuwa na historia kubwa kwenye uwanja wa nyumbani wa Signal Iduna Park.

Dortmund tangu mwaka 2012 ilipokutana na Real Madrid kwenye uwanja huo haijawahi kufungwa mbele ya mashabiki wao, wamekutana jumla mara nne huku Dortmund wakishinda mara tatu na kutoka sare mara moja kabla ya mchezo wa leo, hivyo wana historia nzuri kwenye uwanja wa nyumbani.

Madrid wanashuka dimbani katika harakati za kutetea ubingwa wao waliouchukua msimu uliopita, lakini Dortmund walitolewa kwenye hatua ya robo fainali msimu uliopita.

Katika harakati za kutetea ubingwa Real Madrid walifanikiwa kushinda mchezo wao wa kwanza dhidi ya APOEL kwa mabao 3-0, wakati huo Dortmund wakikubali kichapo cha mabao 3-1 dhidi ya Tottenham Hotspur, lakini katika mchezo wa ligi mwishoni mwa wiki iliyopita, Dortmund iliibuka na ushindi wa kishindo wa mabao 6-1 dhidi ya Borussia Moenchengladbach, wakati huo Madrid wakishinda 2-1 dhidi ya Alaves nchini Hispania.

Katika mchezo huo wa leo Madrid hawajapewa nafasi kubwa ya kushinda ugenini hasa kutokana na kiwango chao msimu huu kuonekana kuwa kipo chini pamoja na Dortmund kubebwa na rekodi ya uwanja wao.

Michezo mingine ambayo itapigwa leo ni pamoja na Napoli ambao watakuwa kwenye uwanja wa nyumbani na kuwakaribisha wapinzani wao, Feyenoord, wakati huo Besiktas ikipambana na RB Leipzig kwenye uwanja wa Vodafone Arena. Sevilla watakuwa kwenye uwanja wao wa nyumbani kuwakaribisha wapinzani wao Maribor.

Tottenham ya nchini England itafunga safari hadi kwenye kiwanja cha GSP ambacho kinaingiza jumla ya watazamaji 22,859, kuwakabili APOEL FC, wakati huo Liverpool wakiwa nchini Urusi kwenye kiwanja cha Otkrytiye Arena kinachoingiza jumla ya watazamaji 45,360.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles