32.2 C
Dar es Salaam
Monday, January 30, 2023

Contact us: [email protected]

Viongozi wanavyokwapua hela za Halmashauri kwa migongo ya vikundi

Na Raymond Minja, Iringa

Diwani wa Kata ya Bumilahinga(CCM), Anderson Mwakyusa na vijana saba wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kushindwa kurejesha fedha za mkopo kiasi cha Sh milioni 52.8 walizokopeshwa na Halmashauri ya Mji Mafinga mkoani Iringa

Hatua hiyo imekuja baada ya kubainika mchezo mchafu unaofanywa na baadhi ya viongozi kusajili vikundi kwa ajili ya kupewa mikopo lakini maara baada ya kupata mikopo hiyo wanagawana na viongozi.

Vijana hao ambao hutumika kama njia ya viongozi kujipatia fedha wamekuwa wakiandika miradi hewa ili mradi tu kujipatia fedha na mwisho wa siku kwenda kugawana.

Akizungumzia sakata hilo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mafinga, Regnard Kivinge amethibisha kukamatwa kwa Diwani huyo pamoja na vijana hao saba kwa kushindwa kurejesha kiasi hicho cha fedha.

“Tunaendelea na jitihada mbalimbali ili kuhakikisha fedha zote walizokopeshwa watu zinarudishwa ili kuvikopesha vikundi vingine.

“Kumekuwa na mchezo na tumekamata hawa vijana hadi walipe kiasi hicho walichokopeshwa au wàeleze namna ambavyo wataweza kulipa mkopo wao na tujue hizo fedha wakipeleka wapi,” anasema Kivinge.

Katika hatua nyingine, Kivinge anasema kuwa sababu iliyopelekea kukamatwa ni kutokana na wataalamu kuvifuatilia vikundi hivyo zaidi ya mara mbili bila mafanikio, hali ambayo ilipelekea kuchukua hatua ya kukamatwa kwa vijana hao ili waweze kujua changamoto iliyosababisha hadi sasa washindwe kurejesha mkopo huo na hata kutokuonekana kwa miradi.

“Wataalamu wetu walianza kuvifuatilia vikundi hivyo ili kujua sababu ya vijana hao kushindwa kurejesha Mkopo ni nini? wakalazimika kutimua nguvu ya ziada ya kuwakamata baada walikiri kushindwa kurejesha fedha hizo kwa madai kwamba Biashara imekuwa nguvu kwao,” amesema.

Kivinge amesema kuwa halmashauri hiyo imekuwa ikitekeleza kwa vitendo agizo la serikali la kukopesha asilimia 10 ya fedha ya mapato ya ndani katika vikundi vya vijana, wanawake pamoja na watu wenye ulemavu kwa mujibu wa sheria ili waweze kuwakwamua kiuchumi.

“Vikundi hivyo vyote viwili vilikuwa vinatoka kata ya Bumilahinga walichukua fedha za mkopo katika halmashauri yetu na ilipitishwa kwa mujibu wa sheria kwa sababu wataalamu wetu walisimamia ili kuhakikisha utaratibu wote unafuatwa,” amesema Kivinge.

Aidha, amevitaja vikundi hivyo kuwa ni kikundi cha kijiji cha Ulole ambacho kilikopeshwa kiasi cha sh milioni 23 Novemba, Mwaka jana huku kikundi cha kijiji cha matanana kilikopeshwa Februari, mwaka huu Sh milioni 29 kwa ajili ya kufanya miradi ambayo waliombea fedha hizo.

“Halmashauri iliwakopesha fedha hizo ili watekeleze miradi ambayo waliandikisha ikiwa biashara ya mbao na uoteshaji ya bustani ya miche ya parachichi kwa kikundi cha Ulole na kikundi cha Matanana kwa ajili ya biashara ya mbao pekee.

“Hawa watu walipewa fedha ila inasemekana kuna michezo michafu ya baadhi ya viongozi kutumia migogo ya vijana kupata fedha kwa kuanzisha vikundi na wakishapata fedha wanakwenda kugawana ndio sababu wanashindwa kurejesha sasa hii tabia inapaswa kukomeshwa mara moja,” amesema Mwenyekiti huyo.

Amesema kuwa endapo vikundi vinashindwa kurejesha mkopo na kutoa sababu ambazo hazionyeshi matumaini ya kurejesha fedha ambazo wamekopeshwa na halmashauri wanahakikisha wanavipeleka mahakamani kwa ajili ya hatua zaidi.

“Tuliamua kuwapeleka polisi ili watoe maelekezo kuhusu fedha hizo na wamezipeleka wapi ukizingatia kiasi hicho ni kikubwa, walipobanwa ndipo wakamtaja Diwani wa kata ya Bumilahinga kuhusika kwenye fedha lakini hata baada ya kuchukua fedha hakuna mabadiliko yoyote,” amesema Mwenyekiti huyo.

Aliongeza kuwa baada ya vijana hao kupelekwa polisi na endapo jambo lolote ambalo litabainika limefanyika kinyume na sheria awe diwani au mtu yoyote sheria itafuata mkondo wake kuhusu sakata hilo.

Kufuatia sakata hilo Kivinge ametoa wito kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga na timu yake kupitia kila kikundi na kujiridhisha kama mchezo huo upo kwenye vikundi vingine vichukuliwa hatua mara moja.

“Kama kuna vikundi vingine ambavyo vinadhani wataweza kuchukua fedha kwa kutumia njia ya udanganyifu sheria haitasita kuwachulia hatua kwa mtu yoyote atakafanya mchezo huo,” anasema.

Mmoja wa waathirika wa upigaji huo kwenye vikundi, Idani Kalinga amesema kuwa ni kweli kumekuwa na badhii ya viongozi kutumia migongo ya vikundi kujipatia fedha na mwisho wa siku wanashindwa kurejesha kutokana na kushindwa kufikiaa malengo

“Ni kweli hiyo michezo ipo mnakubaliana kuunda kikundi na anakuja kiongozi anasema mimi nitahakikisha mnapata mkopo lakini maraa baada ya kupata nyie mtachukua kiasi fulani na mimi nitachukua kiasihiki lakini tutakuwa tunarejesha wote,” anasema mmoja wa wahanga.

Anashauri kuwa ni vyema hizo fedha zinazotolewa kwenye vikundi vikafuatiliwa kwa ukaribu na kuona miradi inayoonekana kwa macho ili kuepuka uhuni unaondelea kwenye baadhi ya vikundi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles