29.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 4, 2023

Contact us: [email protected]

Viongozi wa dini wamchongea Waziri Ghasia

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

VIONGOZI wa dini kupitia Kamati ya Umoja wa Maadili na Haki za Jamii Tanzania wamemtaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amwajibishe

Hawa Ghasia
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Hawa Ghasia

pamoja na uongozi mzima wa Jiji la Dar es Salaam kwa kushindwa kusimamia na kuondoa uchafu uliokithiri kila kona ya Jiji hilo.

Katika barua waliyomwandikia Waziri Mkuu Pinda na MTANZANIA kupata nakala yake, viongozi hao walisema Dar es Salaam ni kioo cha nchi na inapaswa kuwa mfano kwa majiji yote nchini, lakini hali ni tofauti.

Barua hiyo iliyosainiwa kwa pamoja na viongozi watano wakiongozwa na Askofu William Mwamalanga, ilisema wageni wanaoingia jijini humo hulakiwa na harufu mbaya ya uchafu na haijulikani wanaporudi kwao wanaisemaje Tanzania.

“Ni ukweli ulio wazi kwamba manispaa zote za Jiji la Dar es Salaam zimeshindwa kuonyesha jitihada zozote kukabiliana na uchafu kama walivyo wenzetu wa majiji ya Lagos (Nigeria), Cape Town, Johannesburg (Afrika Kusini), Beijing, Hong Kong (China), New York na kwingineko.

“Usafi wa majiji hayo ni matokeo ya uwajibikaji kwa watu waliopewa dhamana,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Katika tamko hilo, pia waligusia wafanyabiashara ndogondogo (machinga) kwamba serikali imetengeneza vita katika miji kwa kushindwa kuwatafutia ufumbuzi wa kudumu ambao sasa wamegeuka kuwa adui wa serikali.

Walisema Serikali imeshindwa kubuni njia mbadala za kuwafanya wamachinga kuwa rafiki wa miji kwa kufanya usafi katika maeneo wanayofanyia biashara.

“Sisi viongozi wa madhehebu ya dini hatukubali kabisa halmashauri za miji, majiji na wilaya kuwageuza wanadamu kuwa sehemu ya uchafu, huo mtindo ni haramu, vijana hawa mwishowe watageuka chanzo cha uhalifu na tunatengeneza vita katika miji yetu,” ilisema sehemu ya tamko hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles