27.7 C
Dar es Salaam
Saturday, June 10, 2023

Contact us: [email protected]

VIONGOZI CHADEMA HEKAHEKA POLISI


Patricia Kimelemeta na Leonard Mang’oha – Dar es Salaam

KUITWA polisi mara kwa mara kwa viongozi wa Chadema kuhojiwa juu ya maandamano waliyofanya Februari 16 na kutawanywa na jeshi hilo, kumeonekana kuwakera.

Kwa mara ya kwanza viongozi hao waliitwa na kuripoti Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam Februari 20, mwaka huu ambako walihojiwa na kutakiwa kurudi tena Februari 27.

Machi 12 na Machi 16, mwaka huu waliripoti tena kituoni hapo na jana ikiwa ni mara ya tano, walienda kuhojiwa kisha kutakiwa kurudi Machi 27.

Viongozi ambao wamekuwa wakitakiwa kuripoti polisi ni Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu, Dk. Vincent Mashinji, Naibu Katibu Mkuu Bara, John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu na Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche.

Wengine ni Mwenyekiti wa Wanawake (Bawacha), Halima Mdee na Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko.

Karibu mara zote ambazo wamekuwa wakiripoti polisi, viongozi hao hawajawahi kufika wote saba kwa pamoja, kutokana na kile ambacho huelezwa ni wengine kuwa kwenye shughuli za kibunge ama kuumwa.

Hali hiyo, jana iliwaponza Mnyika na Heche, ambao wakati wenzao waliripoti na kuachiwa, wao walishikiliwa kwa muda kutokana na kushindwa kufika Machi 16 kama walivyotakiwa.

Pia kutokana na kutohudhuria kituoni hapo jana, Mdee na Matiko wametakiwa kukamatwa na polisi popote walipo.

HALI ILIVYOKUWA JANA

Jana Mbowe, Mashinji, Mnyika, Mwalimu na Heche, walifika katika Kituo Kikuu cha Polisi saa 3:30 asubuhi na kuelekea moja kwa moja ofisi za maofisa wa Jeshi la Polisi ili kujua kinachoendelea.

Ilipofika saa 5:30 …

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya MTANZANIA.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,414FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles