29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 6, 2023

Contact us: [email protected]

Vibaka wamliza Harmonize

harmonizeNA MWANDISHI WETU

MSANII kutoka lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Rajabu Abdulkhali ‘Harmonize’, amewashukuru wakazi wa Tanga kwa kujitokeza kwa wingi kwenye onyesho lake la kwanza alilolifanya mkoani humo siku ya Krismasi licha ya watu wasiofahamika kumuibia vitu vya thamani.

Akizungumzia onyesho hilo, Harmonize alisema hakutarajia kupata mapokezi makubwa kama aliyoyapata, lakini anasikitika baadhi ya mashabiki wasio waaminifu waliweza kumuibia cheni na saa.

“Baada ya onyesho nilishuka chini ili nipige picha na mashabiki wangu, lakini ghafla kukawa na msongamano wa watu nilipokuja kukaa sawa nilijikuta nimepoteza saa na cheni zangu nilizovaa,” alisema Harmonize.

Aliongeza kwa kuwataka mashabiki wake wa Dodoma kujipanga kupokea burudani siku ya Alhamisi kwenye Ukumbi wa Club 7 kwa kuwa ameamua kufunga mwaka mkoani humo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles