Ali Kiba ampagawisha Jokate

0
1342

PhotoGrid_1443334663463NA CHRISTOPHER MSEKENA

NYOTA wa muziki wa kizazi kipya nchini, Jokate Mwegelo, amemsifu msanii mwezake Ali Salehe ‘Ali Kiba’ kwa kutumbuiza muziki na ‘live Band’ kitu kinachoongeza mvuto kwenye maonyesho yake.

Akizungumza na MTANZANIA, Jokate alisema Ali Kiba ni mfano wa kuigwa kwa sababu muziki unakua na soko la kimataifa linahitaji wasanii wanaotumia ala za muziki wawapo jukwaani.

“Ali Kiba ni mfano wa kuigwa, wasanii tusipende kutumia CD kwenye majukwaa tunadumaza vipaji vyetu ni vyema tukafahamu mashabiki pia wamechoka mtindo wa ‘Play Back’,” alisema Jokate.

Aliongeza kuwa alishawishika kuhudhuria onyesho la Funga Mwaka na Ali Kiba kwa sababu alijua burudani inayotolewa na msanii huyo huwa ni ‘live’ kwa kutumia ala za muziki.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here