22.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

VETA kuanzisha mfumo wa mafunzo kwa vitendo

*Lengo ni kwenda sambamba na Teknolojia ya Viwanda

Na Hadia Khamis, Mtanzania Digital

MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imesema inajikita kuanzisha mfumo wa mafunzo ya vitendo ili kwenda sambasamba na teknolojia ya viwanda.

Hayo aliyasema leo Julai 3, 2022 na Mwenyekiti wa Bodi ya VETA, Peter Maduki katika Maonyesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa Dar esSalaam (DITF) alisema mafunzo hayo yatawasaidia wanafunzi kuweza kujiajiri wenyewe na si kusubiri kuajiriwa.

Maduki amesema huo ni mpango wa miaka mitano ambapo hadi sasa vyuo vinne vimejiunga katika mpango huo wa mafunzo ya itendo katika baadhi ya viwanda vilivyopo nchini.

Aidha, amesema mwaka jana mafundi watano walifaulu katika mpango huo na kwa sasa wamejiajiri wenyewe.

Pia amesema lengo lao ni kufundisha wanafunzi 700,000
Lakini hivi sasa jumla ya wanafunzi 300000 wamenfaika na mafunzo.

Naye, Kaimu Mkurugenzi wa VETA, Antony Sekelo amebainisha kuwa lengo la kuwepo katika maonyesho hayo ni kuwapatia watanzania fursa ya kujifunza na kuona jinsi veta inavyoendeleza teknolojia yake.

Amesema kwa sasa Rais Samia Suluhu Hassan amefanya filamu yake ya Royal Tour ambapo veta imeunga mkono jitihada hizo kwa kuanzisha sehemu ya utalii katika chuo chao.

“Veta ina sehemu yake ya utalii ambapo wanafunzi wetu wanapata fursa ya kwenda katika hotel yetu ya Arusha ambayo yenye hadhi ya nyota tatu,” amesema.

Amesema mbali na hoteli hiyo pia wanafundisha namna ya uchimbaji wa madini pamoja na masuala ya gesi, kilimo na viwanda.

Aidha, aliwataka wawekezaji kuwekeza Tanzania kwani wanaowanafunzi wazoefu na waliobobea Katika masuala ya viwanda na utalii

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles