22.1 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

Balozi Dk. Bana, maofisa watembelea miradi ya Dangote Nigeria

Na Mwandishi Maalum, Nigeria

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Nigeria, Dk. Benson Bana na maofisa wa Ubalozi wametembelea mji wa viwanda wa Kampuni ya Dangote (Dangote industrial city) katika jiji la Lagos nchini hapa.

Mji huo unajumuisha ujenzi wa mitambo mikubwa ya kisasa ya kusafisha mafuta ghafi, kiwanda cha mbolea, kiwanda cha kuzalisha plastiki (petro-chemical) na bandari binafsi ya meli za mizigo ambapo mmiliki wake ni mfanyabiashara na tajiri namba moja barani Afrika, Alhaji Aliko Dangote, raia wa Nigeria.

Tajiri huyo amewekeza nchini Tanzania kwa kujenga kiwanda cha kuzalisha saruji katika mkoani Mtwara, ambapo pamoja na mambo mengine, ziara hiyo ilikusudia kuendeleza uhusiano mwema kati ya Tanzania na kampuni ya Dangote, pamoja na hilo Balozi Bana aliishukuru kampuni hiyo kwa kuwekeza nchini Tanzania na aliusihi na kushawishi uongozi wa Dangote kuona uwezekano wa kuongeza uwekezaji wake nchini Tanzania hususani Ujenzi wa Kiwanda cha Mbolea kutokana na uwepo wa gesi ya kutosha.

Aidha, alimpongeza Mwenyekiti wa Kampuni za Dangote, Alhaji Aliko Dangote kwa kufanya ziara nchini Tanzania, Mei 24, mwaka jana ambapo alikutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Alimpongeza kwa ahadi yake kuwa popote atakapokwenda duniani atawashawishi wafanyabiashara wenye mitaji kuwekeza Tanzania kutokana na maboresho anayoyafanya Rais Samia Suluhu Hassan katika mawanda ya uwekezaji na biashara.

Aidha, Balozi alimsihi Alhaji Dangote kutekeleza nia yake ya kuwekeza katika uzalishaji mbolea nchini Tanzania.

“Hatua zinazochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika kuboresha mazingira ya kufanya biashara Tanzania ili kuwavutia wawekezaji na mitaji zinakwenda kuleta mageuzi ya kweli na mazingira salama kwa wekezaji katika nchi yetu,” amesema Balozi Dk. Bana

Kwa upande wa Uongozi wa kampuni ya Dangote, ulimweleza Balozi kuwa nia ya kujenga kiwanda cha mbolea nchini Tanzania bado ipo na kwamba kampuni hiyo itaendelea kupanua miradi yake katika nchi mbalimbali barani Afrika, ikiwemo Tanzania.

Ilielezwa kuwa, hatua za awali hasa utafiti wa ujenzi wa bandari (jet) kwa ajili ya uwekezaji huo, zilishafanyika na mpango wa kuutekeleza unaendelea.

Pamoja na hilokampuni hiyo imekamilisha ufungaji wa mitambo ya kusafisha mafuta na iko katika hatua za mwisho kukamilisha uhakiki wa mitambo ya kusafisha mafuta. Lengo ni kuanza usafishaji mafuta mwishoni mwa mwaka 2022. Kiasi cha cha pipa za mafuta gafi 650,000 sawa na lita 102,700,000 zitasafishwa kwa siku.

Mafuta yatakayokuwa yanazalishwa yatakuwa kwa ajili ya soko la ndani na nje ya Nigeria. Uwekezaji katika mradi huo wa kusafisha mafuta wenye jumla ya miradi 19, unatarajia kuwa wa thamani ya Dola za Marekani zaidi ya bilioni 20. Idadi ya wafanyakazi 20,000 hadi 50,000 waliajiriwa katika hatua mbalimbali za ujenzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles