Vardy aongezewa mkataba Leicester City

0
679

football-leicester-citys-jamie-vardy-celebrates-after-scoring-their-first-goalLondon, England

MSHAMBULIAJI hatari wa klabu ya Leicester City, Jamier Vardy, ameongezewa mkataba wa miaka mitatu na nusu na klabu hiyo ambao utamweka hapo hadi mwaka 2019.

Klabu hiyo imefikia hatua hiyo baada ya mchango wake wa kupachika mabao na kuongoza katika safu ya ufungaji nchini England na klabu hiyo kuwa kileleni katika msimamo wa ligi ambapo hadi sasa ina jumla ya pointi 53 ikifuatiwa na Tottenham yenye pointi 48.

“Ni jambo la furaha kubwa kuwa mtu muhimu katika klabu, ninaamini haya yote yanatokana na kujituma kwangu na ndiyo maana klabu ipo tayari kuwa na mimi.

“Sikudhani kama ningeweza kupata nafasi kubwa katika klabu hii, lakini kutokana na kukubaliana na mmiliki wa klabu, makocha na mashabiki nimepewa mkataba ambao ni kitu muhimu sana kwangu.

“Leicester ilionekana kama haina kitu chochote tangu miaka mitatu na nusu iliyopita, lakini leo hii imenipa jina kubwa na siwezi kuisahau katika maisha yangu kwa kuwa imenifanya niwekeze,” alisema Vardy.

Klabu hiyo ilimsajili mchezaji huyo mwaka 2012 akitokea klabu ya Fleetwood kwa kitita cha pauni milioni 1, lakini kwa sasa atakuwa analipwa pauni 80,000 kwa wiki.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here