22.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

Mourinho: Nitarudi uwanjani hivi karibuni

jose_mourinho_1773090bLONDON, ENGLAND

ALIYEKUWA kocha wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho, amedai kwamba anatarajia kurudi uwanjani muda si mrefu.

Kocha huyo alifukuzwa na klabu ya Chelsea, Desemba mwaka jana kutokana na mwenendo mbaya wa klabu hiyo huku wakiwa mabingwa watetezi.

Hata hivyo, Mourinho amedai kwamba hana furaha hata kidogo kukaa nje ya uwanja bila kufundisha timu, hivyo anatarajia kurudi kwenye soka muda mfupi ujao.

“Sifurahii na maisha haya kwa sasa, kila mmoja anajua jinsi gani ninavyopenda soka, lakini kwa sasa nipo mbioni kurudi uwanjani.

“Ninapenda vitu vingi kama vile familia yangu, marafiki zangu na soka, naweza kuvipenda vyote hivyo na sitaki kukikosa kimoja kati yake.

“Ili niwe na furaha na amani lazima nivipate vyote nivipendavyo kwa wakati, kutokana na hali hiyo ninatarajia kurudi kwenye soka muda si mrefu kwa kuwa nimeanza kuwa kocha tangu mwaka 2000 lakini nilipumzika mara baada ya kuachana na Chelsea mwaka 2007 kwa muda, hivyo sioni sababu ya kuendelea kuwa nje,” alisema Mourinho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,717FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles