28.6 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

Uzinduzi wa SPARK 20 Pro+ Waambatana na zawadi za thamani ya Sh 300,000 kwa kila mwanachuo

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Kampuni ya simu za mkononi TECNO Mobile Tanzania kwa kushirikiana na kampuni ya Mawasiliano Airtel Tanzania wamezindua TECNO SPARK 20 Pro+, SPARK 20 Pro na SPARK 20.

Uzinduzi huo umefanyika Januari 6, mwaka huu katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam ambapo kampuni hiyo iliweka kiingilio cha Sh 10,000 kwa kila aliyehudhuria uzinduzi huo.

Akizungumza na waandisha wa habari wakati wa hafla hiyo Meneja Masoko wa Tecno Tanzania, Salima Shafii alieleza kuwa, “Tumefuraishwa na muitikio huu, waliojitokeza ni wengi kushuhudia uzinduzi wa simu zetu za SPARK 20 Series pamoja ya kuwa tumeweka kiingilio cha shilling 10,000 shukrani nyingi sana kwa wadau wa simu za TECNO mnazidi kutupa nguvu ya kuja na simu zenye teknolojia za kisasa kama ilivyo kwa SPARK 20 series.

“SPARK 20 Pro+ pamoja ya kuwa na bei rafiki lakini unapata simu yenye ufanisi mkubwa wa MediaTek Helio G99, Camera ya Megapixel 108 ikiwa na teknolojia ya ‘9 in 1’ kwajili ya kung’arisha picha zaidi wakati wa usiku na muundo wa 3D Curved,” amesema Shafii na kuongeza kuwa;

“Katika hali ya kurudisha fadhila kwa waliofika siku ya leo, tumewazawadia zawadi zenye thamani ya Sh 300,000 (TECNO earpads, voucher ya manunuzi ya punguzo la asilimia 20 airtel WIFI pamoja na kurudisha shilling 10,000 ambayo ilitumika kama kiingilio hadi hapa sasa nadhani mtakuwa mmelewa dhumuni si kuwatoza pesa wateja wetu bali nikuonyesha upendo kwa wale wenye kutuamini. SPARK 20 Pro+ ipo madukani kwa bei ya shilling 672,600, SPARK 20 Pro 578,200 na Sh365,800 SPARK 20,” alisema.

SPARK 20 Series inapatikana katika maduka yote ya simu nchini Tanzania kwa bei tajwa hapo juu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles