22.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 14, 2024

Contact us: [email protected]

Wafanyakazi Kilimanjaro Express wasekwa ndani, Latra yapigilia msumari

Na Safina Sarwatt, Kilimanjaro

Mkuu wa Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, Kisare Makore ameagiza kuwekwa ndani kwa wafanyakazi wanne wa kampuni ya mabasi ya Kilimanjaro Express kwa kosa la kukatisha tioketi ilihali wakijua kuwa mabasi 35 ya kampuni hiyo yamestishiwa leseni na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini(LATRA).

Itakumbukwa Januari 6, mwaka huu, LATRA ilitangaza kustisha Leseni ya mabasi 35 ya kampuni hiyo kusafirisha abiria kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo kukiuka masharti ya leseni ikiwamo kutotoa tiketi ya kielektroniki na kuzidisha nauli kwa abiria.

Zuio hilo lilitangazwa na Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, Habibu Suluo baada ya kufanya ukaguzi wa kushtukiza katika stendi ya mabasi ya Magufuli pamoja na ofisi za mabasi ya kampuni hiyo ya Kilimanjaro zilizoko Shekilango Dar es Salaam.

Nini kimetokea

Mapema leo, kabla ya Mkuu huyo wa Wilaya kutoa uamuzi huo abiria wa mabasi ya Kilimanjaro Express kutoka Moshi kwenda jijini Dar es Salaam zaidi ya 200 walisota kwa saa sita bila usafiri kwenye ofisi za kampuni hiyo zilizopo mjini Moshi.

Kwa mujibu wa abiria hao ambao tayari walikuwa wamekata tiketi zao walisota katika ofisi hizo kusubiri magari bila mafanikio huku wakiendelea kuambiwa na wafanyakazi wa kampuni hiyo kuwa mabasi yangewasili muda si mrefu kwa ajili ya kuwasafirisha licha yz ukwei kuwa huduma zake zimstishwa na LATRA.

Kufuatia mkwamo huo Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kisare Makore alifika katika ofisi hizo za Kilimanjaro Express na kuamuru abiria hao warudishiwe nauli zao huku hatua zingine zikiendelea kuchukuliwa.

“Kuna sheria ilipitishwa na Bunge kwa watoa huduma ya usafrishaji kutoa tiketi za mtandaoni, hawa Kilimanjaro Express wamegoma, wamedinda, wao wana sheria zao hawataki kufuata sheria zilizowekwa,” alisema Makore.

Makore aliweka wazi kuwa wenye mabasi hayo wamekuwa wakikiuka taratibu za usafrishaji ikiwamo kuwatoza nauli kubwa abiria wanaoanzia safari zao Moshi Mjini kwenda Dar es Salaam Sh 44,000 ambayo ni nauli ya abiria anayeanzia safari zake Arusha badala ya Sh 37,000 kwa mabasi ya daraja la kawaida.

Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kisare Makore(mwenye shati la draft) akizungumza na baadhinya abiria

Utapeli mwingine ambao DC ameutaja ni abiria kupewa tiketi zisizo na namba za mabasi na hivyo kupandishwa kwenye mabasi ambayo hayaendani ya nauli waliyotozwa huku wakilipishwa nauli kubwa ambayo kwenye tiketi inaandikwa pungufu.

“Ulanguzi wa tiketi ni wizi kama wizi mwingine, haiwezekani mtu anasafiri kutoka Moshi kwenda Dar es Salaam anatozwa nauli sawa na mtu anayeanzia safari yake Arusha kama serikali hatuwezi kuruhusu mambo ya kitapeli namna hiyo,” amesema Makore.

Wafanyakazi walivyowekwa ndani

Wakati Mkuu huyo wa wilaya akiingia kwenye jengo la Hotel ya Kilimanjaro ambako ndipo ofisi za mabasi hayo zilipo, wafanyakazi wa kampuni hiyo waliokuwa wakiendelea na zoezi la kurejesha nauli za abiria, ghafla walitoweka na wengine kujificha chooni huku wengine wakikimbilia kwenye baadhi ya vyumba vya kulala wageni hatua iliyomlazimu mkuu huyo wa wilaya kumwagiza OCD kuwatia mbaroni wafanyakazi wanne waliobaki.

Hatua hiyo imetokana na wamiliki wa mabasi hayo kuendelea kuwakatia tiketi abiria huku wakijua kuna katazo na baada ya abiria kuona hakuna kinachoendelea wakampigia simu mkuu huyo wa wilaya.

Baada ya kufika na kukuta watu wa kutosha, akazungumza na abiria na hakusita kusema wazi kuwa kinachofanywa na wenye mabasi hayo ni wizi kama wizi mwingine.

LATRA yaweka kambi

Kuanzia asubuhi ya leo maofisa wa LATRA wakiongozwa na Ofisa Mfawidhi Mkoa wa Kilimanjaro, Paul Nyello walikuwa wamepiga kambi kwenye ofisi za mabasi hayo kuhakikisha hakuna basi linapakia abiria .

Nyello amesema kuwa mabasi hayo yamekuwa yakifanya makosa ya mara kwa mara na licha ya wamiliki wake kuandikiwa barua mara kwa mara za onyo na hata kuitwa na kupewa elimu wamekuwa wakikaidi maelekezo yao.

Ameongeza kuwa makosa yamekuwa yakijirudia mara kwa mara ikiwamo kuzidisha nauli tofauti na nauli elekezi ambako baadhi ya abiria hutozwa nauli kubwa isiyoendana na kiwango halisi huku pia mabasi wanayopakizwa siyo madaraja husika pamoja na kutotoa tiketi za mtandaoni.

“Kama mnavyojua mabasi 35 ya kampuni hii ya Kilimanjaro yamezuiwa kutoa huduma kutokana na makosa mbalimbali na tumekuwa tukiwaita kwa maana ya ofisi zetu za makao makuu na sisi huku mikoani na kuandikiwa barua mara kwa mara na kupewa onyo lakini hawakuwa tayari kubadiliki,” amesema Nyello.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles