29.6 C
Dar es Salaam
Saturday, May 21, 2022

Uwanja wa Ihefu wafanyiwa marekebisho

Na GLORY MLAY-DAR ES SALAAM

UONGOZI wa klabu ya Ihefu, umesema wameanza kuboresha Uwanja wao wa nyumbani wa HighLand Estates, kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Katibu Mkuu wa timu Fredy Chalamila, alisema mechi tatu za mwanzo hazitachezwa kwenye uwanja huo bali wattaumia ule wa Sokoine.

Alisema wanafanya marekebisho katika ujengaji wa kuta, Majukwaa na vyumba vya kubadilishia nguo wachezaji. 

“Tumeshaanza marekebisho ya uwanja huu na mechi tatu za mwanzo hatutautimia kwasababu utakuwa bado haujakamilika, tutatumia uwanja wa  Sokoine, marekebisho yanaendelea na matumaini yetu tutaumaliza mapema,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
191,701FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles