29.6 C
Dar es Salaam
Saturday, May 21, 2022

Simba Queens, Mlandizi kukinukisha Simba Day

Na GLORY MLAY-DAR ES SALAAM

MABINGWA wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara, Simba Queens,inatarajiwa kushuka dimbani leo dhidi ya Mlandizi Queens, katika mchezo wa utakaochezwa kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Simba Queens wanacheza mchezo huo kuwasindikiza kaka zao, katika tamasha maalumu la Simba Day ambalo hifanyika kwa lengo la kuwatambulisha wachezaji wapya. 

Akizungumza na MTANZANIA  jana, Kocha wa Simba Queens, Musa Hassan ‘Mgosi’, alisema timu yake imefanya maandalizi mazuri na wanaamini watawafunga wapinzani wao katika mchezo huo.

 “Tupo vizuri wachezaji wana ari ya kucheza mechi hiyo mele ya umati wa mashiki wetu hivyo tunajitahidi kuahkikisha tunashindana mchezo huo, itakuwa ni aibu tukifungwa,” alisema.

Kwa upande mwingine timu ya Simba ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (U-20), inatarajiwa kuvaana na Fountain Gate.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
191,701FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles