29.4 C
Dar es Salaam
Sunday, October 13, 2024

Contact us: [email protected]

UWT YATOA NENO KWA WANAWAKE WA CCM


Na Elizabeth Kilindi, Njombe

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wanawake (UWT), Gaudencia Kabaka, ameziagiza jumuiya za umoja huo ngazi za matawi, kata, wilaya na mikoa kuanzisha miradi ya maendeleo ili kuiwezesha jumuiya hiyo kujitegemea kiuchumi.

Rai hiyo imetolewa juzi wakati wa ziara yake mkoani Njombe yenye lengo la kuimarisha jumuiya na Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambapo pia aliwashauri wanawake kushiriki uchumi wa viwanda kwa vitendo.

“Mkoa wa Njombe ardhi yake inakubali kila kitu, msiogope kuanzisha viwanda vidogo vidogo maana nimeona kuna matunda mengi ambayo pia ni fursa,” alisema Kabaka.

Kabaka alisema ni wakati wa jumuiya hiyo kujitegemea na kuwa miradi yake itasaidia kuinuka kiuchumi na kuacha kuwa tegemezi.

“Kwa awamu hii hatutakiwi kulalamika kwamba hatuna fedha, lazima tuanzishe miradi ambayo itatusaidia kuendesha shughuli za jumuiya yetu,” alisema Kabaka.

Kabaka aliwataka wanawake mkoani humo kuiamini CCM ili kuweza kuipa ushindi uchaguzi ujao wa Serikali za mitaa na hivyo kuondoa tofauti zilizokuwepo katika uchaguzi uliopita.

Mwenyekiti wa jumuiya hiyo Mkoa wa Njombe, Rosemary Rwiva, aliwataka wanawake kujiunga na mfuko wa CHF ili kupata matibabu kwa urahisi.

“Wanawake wahimizeni wanaume zenu ili wote mjiunge na CHF mpate matibabu kwa urahisi… Tujali afya zetu ili tuweze kuzisimamia familia zetu,” alisema Rosemary.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles