23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Utunzi wa mitihani uzingatie uwezo wa watoto kiakili

Wanafunzi wakifanya mtihani.
Wanafunzi wakifanya mtihani.

MWANANGU alipokuwa kidato cha tatu, siku moja akaniletea maswali ya mtihani aliofanya shuleni kwao na akaniomba nimsaidie ili afanye masahihisho. Swali lenyewe lilikuwa hivi: “Make critical analysis of factors that led to the rise of capitalist economy in the world!” Ninapoandika makala haya mwanangu huyo ana miaka 19. Na amemaliza kidato cha nne miaka miwili iliyopita, kwa hiyo alikuwa na miaka 15. Unaweza kweli kumpatia swali zito la namna hiyo mtoto wa miaka 15? Swali ambalo mtoto wa chuo kikuu linaweza kumtoa jasho jingi!

Ni kwanini nilililalamikia swali hili kuwa halimfai mtoto wa mwaka huyo. Ni kwa sababu watoto wanatakiwa kutambuliwa uwezo wao wa kufikiri kabla ya kusomeshwa. Ingawa kuna tofauti kati ya malezi lakini tunafahamu kuwa katika umri wa miaka 15 watoto wengi hawajejenga bado uwezo wa kufikiri kwa udhahania – abstract thinking… na kuwa wengie wanaouwezo wa kukariri kwa kusaidiwa na vitu hali au matukio halisi wanayoyaona au kuyasikia. Ingawa wanaweza kusoma hadithi lakini wanapozifikiria wanafikiria katika mfumo wa vitu halisi. Unapomtaka mtoto afanye “critical analysis” maana yake unataka afanye tafakuri ya uwezo wa juu unaojumuisha kwanza uchambuzi wa vipengele vya jambo husika, na pili kuviunganisha na kuona namna gani vinasaidiana katika kulijenga jambo – analysis and synthesis, halafu aweze kuona kama kuna kasoro au mapungufu…uwezo huu ni wa mtoto aliyefikia umri wa kuweza kufanya tafakuri ya kiwango cha juu namna hiyo.

Hoja hii inatukumbusha kuwa kila wakati unapoandaa somo lako; unapoandaa mazoezi ya vitendo ay ya kujadili kwa vikundi; au unapoandaa mitihani na kila aina ya shughuli itakayofanywa na wanafunzi wako, fikiria uwezo wao wa akili umifikia kiwango gani kwa ujumla…katika kuweza kuchakata taarifa na kuzitolea majibu au maoni. Kuna uhusiano mkubwa kati ya uwezo wa wanafunzi kuyashika wanayofundishwa na maarifa wnayobaki nao. Kunaweza kutokea tofauti kati ya mwanafunzi mmoja mmoja lakini, kimsingi ni kuwa katika kundi moja la wanafunzi wa darasa moja, uwezo wao wa akili huweza kufanana.

Mara nyingi tunaposikia watoto wamefeli kwa wingi katika mitihani ya darasa la nne, la saba au kidato cha nne, moja ya sababu tunayotakiwa kujiuliza ni kama mitaala ya elimu, mihutasari ya masomo, na mtindo wa ufundishaji, hatimaye utunzi wa maswali yenyewe vilizingitia uwezo wa akili katika kila rika – au umri. Tukifanya utafiti wa kisaikoloji katika eneo hili tunaweza kupata majibu mengi…tatizo letu ni kuwa hapa Tanzania, linapotokea tatizo kama hilo la wanafunzi kufeli kwa wingi, tunaanza na majibu ya kisiasa badala ya kitaaluma, na hapa ni kisaikolojia. Nilidhani ili tuweze kujua namna gani tunaweza kuongoza elimu, wataalamu wetu wafanye utafiti juu ya umri wa jumla na uwezo wa jumla wa wanafunzi wetu katika ngazi mbalimbali za elimu, na baadaye watueleze kuwa tofauti hizo za umri katika ngazi mbalimbali zinahitaji sisi tufanye nini ili kutunga mitihani, vitabu, na kufanya mafundisho sahihi kabisa.

Lakini walimu wenyewe wanaweza kufanya utafiti wao bila kusubiri wataalamu na serikali. Walimu wengi wamejifunza juu ya kukua kwa watoto- growth and development- na hivyo wanaweza kujua kuwa watoto wanaowafundisha wako katika umri gani na katika umri huo watoto hao wanaweza kusoma namna gani na kama kile kilichoko kwenye mtaala na mihutasari na vitabu vinafanana na uwezo wao? Kama ndivyo na yeye afundishe namna gani ili wasipoteane njia na wanafunzi. Tuonane wiki ijayo…

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles