24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

UTEUZI WA KIMKAKATI

Na GRACE SHITUNDU-DAR ES SAALAM          |         


RAIS Dk. John Magufuli amefanya mabadiliko ya uongozi na kujaza nafasi katika baadhi ya wizara, mikoa na wilaya, huku miongoni mwa aliowateua katika nafasi hizo wakiwa ni wanasiasa watatu waliohama upinzani.

Wanasiasa hao ambao walijiunga kwa nyakati tofauti na CCM, ni David Kafulila ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe,  Patrobas Katambi Mkuu wa Wilaya ya Dodoma pamoja na Moses Machali anayekuwa Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu.

Tayari uteuzi huo umeibua mjadala  kwamba kujiunga kwao CCM hakukuwa bure, lakini pia huenda sasa nafasi zao hizo zikawasaidia kujiandaa kisiasa katika chaguzi zijazo.

Katika uteuzi huo ambao Rais Magufuli aliutangaza moja moja kupitia Televisheni ya Taifa (TBC) kutoka Ikulu, jijini Dar es Salaam, mbali na kuwaingiza wanasiasa hao, wapo aliowateuwa kwa mara ya kwanza huku wengine akiwapandisha.

Miongoni mwa viongozi wapya walioteuliwa ni mwanamitindo maarufu nchini, Jokate Mwegelo, ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe.

Jokate ambaye ana ushawishi mkubwa kwenye jamii na mitandao, anachukua nafasi ya Happines Seneda.

Kuteuliwa kwake huko kumekuja baada ya Machi 25 mwaka huu, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM, Hery James kutengua uteuzi wake wa Kaimu Katibu wa Hamasa na Chipukizi wa umoja huo.

WAKUU WA MIKOA

Katika uteuzi huo waliopanda kutoka ukuu wa wilaya hadi mikoa kuziba nafasi zilizoachwa wazi na waliostaafu ni  pamoja na Ally Hapi ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya Kinondoni,  ambaye sasa ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, akichukua nafasi ya Amina Masenza.

Mwingine ni aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Buhingwe, Brigedia Jenerali Gaguti, ambaye sasa ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera akichukuwa nafasi ya Meja Jenerali Salum Kijuu ambaye amestaafu.

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.
- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

  1. toka Geita,
    Yuko sawa, maana yeye ndiye kocha, nasi tushakabidhi kila kitu kwake. Hivo kama Meneja na bench lake la ufundi kaona yafaa kusajili & wazee wapumzike basi na afanye hiyvo…. Siye twataka medali tu.. KILA LA KHERI Mzee Baba ‘JPM’…

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles