24.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 7, 2022

USHAURI HUU UKIFANYIWA KAZI WATOTO NJITI HAWATAPOTEZA MAISHA

Na FERDNANDA MBAMILADAR ES SALAAM


TATIZO la watoto kuzaliwa kabla ya muda wao (njiti) bado ni changamoto kubwa nchini, huku wataalamu wa masuala ya afya wakisema kuwa asilimia 70 huzaliwa hivyo bila kuwapo kwa sababu za kisayansi zinazoonyesha chanzo cha tatizo.

Hivi majuzi, Daktari Bingwa wa Watoto kutoka Hospitali ya Agha Khan, Yaser Abdallah, alibainisha kuwa ni asilimia 30 tu ya watoto hao ndio hujulikana chanzo chake.

Miongoni mwa vyanzo vya mama kujifungua mtoto njiti ni kupata maambukizi katika mfumo wa uzazi au mkojo, kuwa na ujauzito pacha au zaidi na mama kuugua maradhi wakati wa ujauzito kama vile malaria.

Kwa mujibu wa Dk. Abdallah, watoto wanaozaliwa njiti wapo hatarini zaidi kufariki dunia au kupata ulemavu endapo hatopatiwa huduma nzuri za afya mara baada ya kuzaliwa.

Tatizo hili ni kubwa duniani kote, ambapo kwa mwaka watoto milioni moja huzaliwa njiti .

Tofauti iliyopo ni kwamba nchi zilizoendelea wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuokoa maisha ya watoto hawa ukilinganisha na nchi zinazoendelea.

Hivyo basi, ili kuokoa maisha yao, Dk. Abdallah anashauri kuwapo kwa ushirikiano kati ya Serikali na hospitali binafsi zenye vifaa vya kutunzia watoto wa aina hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,859FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles