31 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 3, 2023

Contact us: [email protected]

Usajili alama za vidole; Wateja 157,000 wa Vodacom wafungiwa huduma

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania imewafungia huduma wateja wake 157,000 ambao wameshindwa kujisajili kwa kutumia alama za vidole.

Hatua hii inatokana na agizo la Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), kuziagiza kampuni zote za simu nchini kuwafungia wateja ambao wameshindwa kusajili kwa kutumia alama za vidole ifikapo Januari 20, mwaka huu.

Akitangaza uamuzi huo leo Jumatano Januzri 22, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Hisham Hendi, amewaomba wateja wote waliofungiwa laini zao kutembelea vituo vya huduma au mawakala wa kampuni hiyo zaidi ya 35,000 nchini kusajili laini zao ili kuendelea kufurahia huduma za kampuni hiyo.

“Baadhi ya maduka yetu kwenye miji mikubwa yatakuwa wazi saa 24 ili kuhakikisha wateja wetu wote ambao wana vitambulisho vya taifa wanasajiliwa na hivyo kuendelea kupata huduma za kampuni yetu ikiwa ni pamoja na huduma za M-Pesa,” amesema Hendi.

Amesema wateja walioathiriwa na zoezi hili ni wale tu waliopokea namba za vitambulisho vya Taifa kutoka mamlaka ya vitambulisho hivyo (NIDA), lakini wameshindwa kujisajili kwa sababu moja au nyingine.

“Kwa kuwa zoezi hili ni endelevu, wateja wetu wote ambao hawajapata namba za utambulisho kutoka NIDA, waendelee na mchakato wa kupata namba hizo au vitambulisho vitakavyowawezesha kujisajili kwa kutumia alama za vidole na kuepuka usumbufu wa kufungiwa huduma,” amesema.

Pamoja na mambo mengine, Hendi amesema zoezi la usajili kwa alama za vidole litasaidia kupunguza idadi ya matapeli wanaosumbua wateja ambapo itarahisisha vyombo vya usalama kupambana na matukio hayo ya kitapeli.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja, Harriet Lwakatare amesema kwa wale walioathiriwa na zoezi hili la kufungiwa wasiwe na wasiwasi kwa vile taarifa zao zitatunzwa kwa muda wa miezi sita ambapo wanatarajiwa wawe wamejisajili kwa alama za vidole. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles