28.6 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

Chris Brown: Watoto wanabadilisha maisha yangu

New York, Marekani

MKALI wa muziki wa RnB nchini Marekani, Chris Brown, ametumia ukurasa wake wa Instagram na kuweka wazi kuwa, mfumo wa maisha yake umebadilika kwa kiasi kikubwa kutokana na kuitwa baba.

Mwishoni mwa wiki iliopita msanii huyo mwenye umri wa miaka 30, aliposti picha mbalimbali kwenye Instagram akiwaonesha watoto wake wawili Royalty mwenye miaka sita na Aeko mwenye mwezi mmoja.

Watoto hao wote ni mama tofauti, lakini msanii huyo amedai akili yake kwa sasa imetulia kwa kuwa anaitwa baba, hivyo ni lazima awe wa mfano bora.

“Nawapenda wanangu, mfumo wa maisha yangu umebadilika kutokana na uwepo wenu, nitafanya chochote kwa ajili ya kuyapigania maisha yengu wanangu,” alisema msanii huyo.

Royalty alimpata wakati yupo kwenye uhusiano na mwanamitindo Nia Guzman, wakati huo Aeko akimpata wakati yupo kwenye uhusiano na Ammika Harris.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles