30.5 C
Dar es Salaam
Thursday, May 26, 2022

Urusi, Misri kuimarisha  ushirikiano

MOSCOW,  Urusi

URUSI na Misri zimesema zitaendelea kushirikiana katika nynja mbalimbali ili uhusiano baina ya mataifa haya mawili uweze kufika ngazi nyingine.

Taarifa hiyo ilitolewa jana na Waziri wa Mambo ya Nje wa hapa,  Sergey Lavrov kupitia ujumbe aliouandika katika jarida la  Time-Tested Friendship na kuchapishwa katika tovuti ya gazeti la  Al-Ahram  la  Misri.

Lavrov alisema uhusiano  wa siasa kati ya nchi hii na Misri unazidi kukua na biashara baina ya mataifa haya mawili inazidi kuchanua tangu ilipofikia wastani wa dola  bilioni 6.5  kwa mwaka.

“Ushirikiano katika nyanja za jeshi unawezesha vikosi vya Misri na utekelezaji wa sheria kupinga vitisho vya ugaidi kwa ufanisi zaidi,” alisema waziri huyo.

“Aina mpya za ushirikiano katika nyanja hii zinajaribiwa kwa ufanisi.

“Oktoba 2016 katika mkutano uliofanyika katika ardhi ya  Misri na   Septemba 2017 katika  mkutano uliofanyika  Urusi kwa pamoja tulikubaliana  kupambana  dhidi ya ugaidi  na katika mkutano wa utetezi wa urafiki uliofanyika mwaka  2016  na mwaka  2017  ambao ulivihusisha vikosi vya anga vya mataifa haya mawili,”aliongeza waziri huyo.

Alisema Urusi na Misri zimekuwa zikishirikiana kwa karibu katika kutatua migogoro mbalimbali duniani  kujenga umoja miongoni mwa jamii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
192,358FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles