Familia ya yatangaza dau nono kwa atakayempata Mo Dewji

0
1419

Nora Damian, Dar es SalaamFamilia ya mfanyabiashara maarufu na mwekezaji wa Klabu ya Simba, Mohamed Dewji  ‘Mo’ aliyetekwa Alhamisi wiki iliyopita, imetangaza donge nono la Sh bilioni moja kwa atakayefanikisha kupatikana kwa mtoto wao.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Oktoba 15, Msemaji wa familia, Azim Dewji, amesema mtoa taarifa pamoja na taarifa zitabaki kuwa siri kubwa baina ya mtoa taarifa na familia.

“Katika kuhakikisha Mo anapatikana, zawadi nono ya Sh bilioni moja itatolewa kwa yeyote atakayetoa taarifa za kupatikana kwa mtoto wetu, taarifa na mtoa taarifa itabaki kuwa siri ya familia na mtoa taarifa,” amesema Dewji.

Pamoja na mambo mengine, Dewji ameishukuru serikali na taasisi zake kwa jitihada wanazoendelea kuzifanya katika kuhakikisha mtoto wao anapatikana huku akiziomba taasisi za dini kuendelea kuwaombe katika kipindi kigumu familia inayopitia.

Familia ya Mo, imejitokeza hadharani leo ikiwa ni siku ya tano tangu alivyotekwa na watu wasiojulikana katika Hoteli ya Colosseum, jijini Dar es Salaam, saa 11 alfajiri wakati akiingia kufanya mazoezi hotelini hapo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here