31 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 3, 2023

Contact us: [email protected]

Upelelezi baba aliyebaka bintiye wakamilika

Na AVELINE KITOMARY

-DAR ES SALAAM

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar es Salaam, imepanga Juni 24 kumsomea maelezo ya awali Said Rashidi (36) katika kesi inayomkabili akituhumiwa kumbaka binti yake nwenye umri wa miaka 13.

Mwendesha mashtaka, Matarasa Hamisi, alidai mbele ya Hakimu Mkazi Joyce Mushi kuwa upelelezi wa shauri hilo umekamilika.

“Upelelezi wa shauri hili umekamilika, tunaomba tarehe kwa ajili ya kuwasilisha hoja za awali,” alidai Matarasa.

Hakimu Moshi aliahirisha shauri hilo kutokana na maelezo yaliyotolewa na upande wa mashtaka hadi itakapokuja kusomewa hoja za awali Juni 24.

Mshtakiwa alirudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Katika kesi ya msingi, mshtakiwa anadaiwa katika tarehe zisizojulikana kati ya mwaka 2016 na Aprili, 2019 eneo la Mbezi Juu, Wilaya ya Kinondoni, alimbaka mtoto wake mwenye umri wa miaka 13 (jina tunalo).

Wakati huo huo, upande wa mashtaka katika kesi ya utekaji inayowakabili Happyness Gimonge  (22) na James Shayo, umesema upelelezi wa kesi bado haujakamilika.

Wakili Abudi Yusuph aliiomba mahakama kutaja tarehe nyingine kwa ajili ya kukamilisha upelelezi.

“Upelelezi wa shauri hili bado haujakamilika, naiomba mahakama itaje tarehe nyingine kwa ajili ya kukamilisha upelelezi,” alidai Yusuph.

Kutokana na madai yaliyotolewa, Hakimu Boniface Lihamwike aliahirisha shauri hilo hadi Juni 24, mwaka huu huku mshtakiwa wa kwanza Happyness aliachiwa kwa dhamana na Shayo alirudishwa rumande.

Katika kesi ya msingi, washtakiwa wanadaiwa  Mei 6 mwaka huu eneo la Kimara Bonyokwa, Wilaya ya Ubungo,  walimteka Angle Mwita na kumwambia mama yake Christina Massa atume fedha kiasi cha Sh milioni 52 ili kumpata mtoto wake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles