26.1 C
Dar es Salaam
Friday, May 3, 2024

Contact us: [email protected]

UNDANI SKENDO YA DIAMOND, KIBA KUNUNUA VIEWER’S

Na CHRISTOPHER MSEKENA

TUHUMA za kununua watazamaji (viewer’s) wa video zimeendelea kumwandama msanii nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kila anapotoa ngoma mpya.

Wiki hii tuhuma hizo zimehamia kwenye video yake mpya ya Hallelujah aliyowashirikisha kundi kutoka Jamaica, Morgan Heritage ambayo ndani ya siku moja iliweka rekodi ya kutazamwa  na watu milioni 2.

Kwa rekodi hiyo akawa ameikaribia rekodi ya  Saad Lamjarred, msanii kutoka Morocco anayeshikilia rekodi ya video yake ‘Let Go’ kutazamwa na watu wengi kwa muda mfupi kwani ilitazamwa mara milioni 5 ndani ya saa 24 pekee.

Tuhuma za kununua watazamaji zimekuja baada ya watu kutokuwa na uelewa mpana juu ya video vinazowekwa kwenye mtandao ya YouTube chini ya Google na tovuti ya Vevo.

Leo Swaggaz tunakupa madini ya kutosha ili usanuke na kufahamu tofauti ya YouTube na Vevo.

IFAHAMU KWA UFUPI VEVO

Neno Vevo ni kifupi cha ‘Video Evolution’ ambayo ni tovuti iliyoanza kufanya kazi rasmi Desemba 8, 2009, ambayo lengo lake lilikuwa ni kudhibiti wizi wa kazi za wanamuziki wa lebo kubwa duniani uliokuwa unafanyika hasa video.

Vevo ilijidhatiti kusimamia video za wanamuziki wa lebo kubwa tatu duniani ambazo ni Universal Music Group (UMG), Sony Music Entertainment (SME) na Warner Music Group (WMG) iliyojiunga rasmi na Vevo Agosti, mwaka jana.

VEVO HUITEGEMEA YOUTUBE

Huo ndiyo ukweli, hakuna Vevo bila YouTube kutokana na ukweli kwamba tovuti hiyo inapatikana kwenye nchi chache tu duniani ambazo ni Australia, Blazil, France, Germany, India, Ireland, Italia, Uholanzi, Hispania, Thailand, Uingereza na Marekani pekee.

Wakati YouTube inapatikana ulimwenguni kote isipokuwa kwenye nchi ilikozuiliwa kama Pakistan, Syria na China hivyo kuwa ni fursa ya kuwafikia watu wengi wakiwemo mashabiki wa Bara la Afrika ambako hakuna nchi yenye muunganiko wa moja kwa moja na Vevo. Kwa kifupi Vevo ni mpangaji ndani ya YouTube.

VEVO SIYO YA KILA MSANII

Kama nilivyokufahamisha hapo juu kuwa Vevo inasimamia video za wasanii wa lebo za Universal Music Group, Sony Music Entertainment na Warner Music Group na wasanii wachache wanaojitegemea ambao wanalipia kama ushuhuru wa dola 20 kwa mwaka.

Kwa hiyo siyo kila msanii anaweza kuwa na akaunti Vevo, ndiyo maana utaona ni wasanii wawili tu Bongo – Diamond Platnumz na Ali Kiba ndiyo wenye akauti Vevo walizozopata kupitia mwamvuli wa lebo zao za Universal Music Group na Sony Music Entertainment.

UTOFAUTI WA VEVO, YOUTUBE

Tofauti ya kwanza ni kwenye malipo, Vevo inamlipa vizuri zaidi msanii kuliko YouTube kwa kuwa tovuti hiyo hutoza kiasi kikubwa cha fedha kwenye matangazo ya kampuni zinazotangaza na huonyesha matangazo hayo kwa urefu na mara nyingi zaidi.

Tofauti ya pili ipo kwenye maudhui ambapo ndani ya Vevo utazikuta video za muziki na matamasha ya wasanii wale wa zile lebo tatu tu, huwezi kukuta video ambayo haihusiani na muziki.

Wakati kwenye YouTube kuna wigo mpana na ni ruhusa kuweka video yenye maudhui yoyote ambayo hayavunji miiko ya YouTube.

Lakini pia Vevo huendeshwa na lebo zenyewe, msanii hana uwezo wa moja kwa moja kuweka video yake, mfano kama Ali Kiba akiwa na video analazimika kuwatumia Sonny Music Entertainmnt ambao wao ndiyo watamuwekea kwenye akaunti yake ya Vevo.

Wakati YouTube msanii mwenyewe ana uhuru wa kuweka video anavyotaka. Na jambo la mwisho ni kwenye watazamaji (viewers), kama kutakuwa na tofauti basi ni asilimia zisizozidi tano kwa kuwa watazamaji wa Vevo huangalia video kupitia YouTube.

Labla ifanyike janjajanja ya kununua viewers kutoka kwenye kampuni kama Marketing Heaven, ambayo inasifika kwa kuuza  viewer’s, lakini si jambo rahisi kwa msanii anayesimamiwa na lebo kubwa kama Universal Music Group na Sonny Music Entertainment kununua watazamaji kutokana na ulinzi waliowekewa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles