27.5 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

UN yaingilia kati mgogoro wa Gabon

Ali Bongo
Ali Bongo

LIBREVILLE, Gabon

UMOJA wa Mataifa (UN) umehimiza kuwepo utulivu nchini Gabon baada ya fujo kuzuka kutokana na utata kuhusu matokeo ya uchaguzi wa urais.

Baraza la Usalama la umoja huo limetoa wito kwa wagombea wakuu na wafuasi wake kujizuia kufanya uchokozi na kutatua mzozo wa sasa kupitia njia za kisheria.

Hadi sasa, maofisa usalama waliwakamata watu zaidi ya 1,000 baada ya siku ya pili ya maandamano ya wafuasi wa upinzani.

Upinzani unadai kuwa Rais Ali Bongo aliiba kura wakati wa uchaguzi huo uliofanyika Jumamosi.

Rais Bongo alisisitiza kwamba, alishinda kwa njia halali na kuutaja ushindi wake kuwa ushindi wa watu wa Gabon na kwamba kuna kundi dogo la watu wachache waliotaka kutwaa madaraka ambao wameshindwa.

Matokeo ya uchaguzi nchini humo yaliyotangazwa Septemba 31, mwaka huu yalimpatia Rais Bongo ushindi kwa 49.8% ya kura, akifuatiwa na Jean Ping aliyepata 48.2 % ya kura na kufanya kutofautiana kwa kura 5,594.

Ping alisema uchaguzi huo ulijaa udanganyifu na kwamba hakuna ajuaye hasa nani alishinda na kwamba upande wake unaonyesha asilimia 99 ya wapiga kura walijitokeza kupiga kura hivyo ameomba takwimu za wapiga kura kutoka kila kituo zitolewe wazi.

Rais Bongo aliingia madarakani mwaka 2009 baada ya kifo cha baba yake aliyekuwa ameongoza taifa hilo tangu 1967.

Kabla ya kuingia katika siasa, Ping aliwahi kuhudumu kama Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles