29.7 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

UN: Mapigano yamezalisha maelfu ya wakimbizi

TRIPOLI, LIBYA

UMOJA wa Mataifa (UN) umetangaza kuwa zaidi ya watu 90,000 wamekuwa wakimbizi huko Tripoli, mji mkuu wa Libya tangu Jenerali Khalifa Haftar alipoanzisha vita dhidi ya mji huo mwezi Aprili mwaka huu.

Televisheni ya Rusia al Yaum ilimnukuu Msemaji wa Katibu Mkuu wa UN, Farhan Haq, akisema kuwa idadi ya watu waliokimbia makazi yao mjini Tripoli kutokana na mapigano, imeongezeka na kuzidi kiwango hicho kilichotajwa. 

 “Idadi yao inazidi kuwa kubwa siku baada ya siku kiasi kwamba katika kipindi cha wiki moja ya hivi sasa, karibu watu elfu nane wamekimbia makazi yao huku nusu yao wakiwa ni watoto wadogo,” alisema.

Aliongeza kuwa maofisa wa misaada wanaendelea na kazi yao ya kuwasaidia wakimbizi hao kiasi kwamba watu zaidi ya 47,000 wa Tripoli na maeneo ya karibu na mji huo wameshafikishiwa misaada.

Jenerali Haftar alianzisha mashambulizi ya pande zote dhidi ya mji wa Tripoli baada ya kutembelea Saudia na kuonana na viongozi wa nchi hiyo akiwemo Mfalme Salman.

Aprili 4 mwaka huu, Jenerali Haftar alitoa amri ya kushambuliwa Tripoli. 

Jenerali huyo muasi anaungwa mkono na Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu, Misri na Ufaransa. 

Hata Rais wa Marekani, Donald Trump alimpigia simu akitangaza uungaji mkono wake kwa kile alichodai ni kupambana na ugaidi na kulinda usalama wa visima vya mafuta vya Libya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles