21.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, July 23, 2024

Contact us: [email protected]

Umeme siyo anasa, ni hitaji la lazima – Dk. Biteko

Lilian Lundo na Veronica Simba

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko amesema umeme siyo anasa bali ni hitaji la lazima kwa wananchi.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko akifurahia jambo na wakazi wa kijiji cha Nyantakara, Wilaya ya Biharamulo Mkoa wa Kagera mara baada ya kuwasha umeme leo Septemba 27, 2023.

Dk. Biteko amesema hayo leo Septemba 27, 2023 wakati wa hafla wa uwashaji umeme Kijiji cha Mubaba na Nyantakara vilivyopo Wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera.

“Nimewaambia REA pelekeni umeme vijijini, tunataka Watanzania wazoee umeme. Umeme siyo anasa tena bali ni hitaji la lazima kwa Watanzania,” amesema Dk. Biteko.

Ameendelea kusema kuwa, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ameongeza kasi kwenye umeme, na anajali shida za Watanzania, hivyo anatatua changamoto mbalimbali likiwemo suala la umeme.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko akibonyeza kitufe kama ishara ya kuwasha umeme katika katika Kijiji cha Nyantakara, Wilaya ya Biharamulo Mkoa wa Kagera leo Septemba 27, 2023.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy amesema Mkoa wa Kagera una jumla ya vijiji 662 ambapo vijiji 512 sawa na asilimia 77.3% vimepata huduma ya umeme kupitia miradi ya awali ikiwemo REA Awamu ya Tatu Mzunguko wa Kwanza, REA Awamu ya Pili na REA Awamu ya Kwanza.

Ameendelea kusema kuwa, kwa sasa REA inatekeleza jumla ya miradi mitano katika maeneo tofauti ya mkoa wa Kagera, ambayo ni mradi wa REA Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili, mradi wa kupeleka umeme pembezoni mwa miji, mradi wa ujazilizi, mradi wa kupeleka umeme kwenye migodi midogo na maeneo ya kilimo na mradi wa kupeleka umeme kwenye Vituo vya Afya na Pampu za Maji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles