22.3 C
Dar es Salaam
Saturday, July 13, 2024

Contact us: [email protected]

Umati wahudhuria maandamano HongKong licha ya mvua kali

GUANGDONG, HONG KONG

LICHA ya mvua kali iliyokuwa ikinyesha nchini hapa, umati wa watu wakiwamo wazee walijiunga na wanaharakati vijana na wengine wenye msimamo mkali kuandamana jana.

 Waandaaji wanakadiria watu wasiopungua milioni mbili wanashiriki maandamano hayo, idadi ambayo ni kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa tangu mwaka 1997 katika maandamano jimboni humo.

Polisi imeruhusu watu wakusanyike, lakini wasiandamane, lakini waandamanaji wameipuuza amri hiyo na kushiriki kwa wingi mitaani katikati ya Hong Kong licha ya mvua kali.

“Ikiwa mbinu za Beijing na Hong Kong ni kuona vuguvugu letu linadhoofika, wamekosea, hatutochoka,” alisema Bonnie Leung wa shirika linalopigania haki za raia la CHRF.

Waandamanaji wanasema wamepania kuionyesha Serikali kuwa hawatoachana na  madai yao matano ikiwa ni pamoja na kubatilisha muswada wa sheria kuhusu wahalifu kuhamishiwa China na uchunguzi huru kuhusu matumizi ya nguvu ya polisi.

Katika madai yao, waandamanaji hao wanadai pia kiongozi wa Serikali ya jimbo hilo, Carrie Lam ajiuzulu.

“Tutabakia hapa hapa, tutasimama kidete hadi wanatujibu. Kwa pamoja tuna nguvu zaidi,” alisema mwanafunzi Harles Ho.

Kijana huyo wa miaka 20 alisema mvua kali haitobadilisha msimamo wao.

Wakati matumizi ya nguvu yaligubika maandamano yao wiki za hivi karibuni, waandaaji wa maandamano ya jana walitaraji kudhihirisha kwamba wakaazi wa Hong Kong wanaweza kuandamana kwa amani.

Waandamanaji walikosolewa wiki hii baada ya maandamano katika uwanja wa ndege wa kimataifa kumalizikia kwa mapigano dhidi ya  polisi wa kuzuia fujo.

Katika tukio hilo, waandamanaji hao waliwazuia abiria wasisafiri na baadaye kuwavamia watu wawili waliokuwa wakiwatuhumu kuwa majasusi wa Serikali kuu ya China.

Picha hizo ziliichafua taswira ya waandamanaji hao na kusababisha baadhi ya waandaaji kuomba radhi.

Vuguvugu la maandamano lilianza Juni 9, mwaka huu katika jimbo hilo la HongKong lililokuwa zamani likisimamiwa na Uingereza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles