27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, July 24, 2024

Contact us: [email protected]

Kamera za usalama kufungwa vituo vya ukaguzi

Janeth Mushi -Arusha

MKUU wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo,amesema Serikali itaweka kamera katika vituo vinne vya ukaguzi wa magari ya utalii mkoani hapa kwa lengo la kufuatilia na kupunguza usumbufu barabarani.

Alisema yeye siyo aina ya viongozi wanaoona ufahari kufukuzisha mtu kazi, badala yake kuwataka polisi kikosi cha usalama barabarani kuzingatia utaratibu uliowekwa, ikiwemo kutokusimamisha mara kwa mara magari ya utalii labda kuwe na taarifa za vitendo vya uhalifu.

Alisema hayo juzi jijini hapa, alipozungumza wakati wa kikao kazi na askari wa mkoa huo.

Alisema wamechoka malalamiko yanaypotolewa na baadhi ya wadau wa utalii dhidi ya askari wa usalama barabarani na kuwa baada ya kujengwa kwa vituo hivyo ambavyo viko maeneo ya Kikatiti,Makuyuni,Karatu na Engikareti,watafunga kamera ili kuona matukio yanayofanyika.

“Huu ni mfumo maalumu ambao utaondoa lawama,ikizingatiwa sekta ya utalii inachangia kiasi kikubwa cha mapato,hatusemi mtu akibeba watalii aachwe hapana, magari hayo yasimamishwe kwenye vituo vinne tu ila kama kuna kesi maalumu muyakague kwa sababu wengine wanaweza kuyatumia kufanya uhalifu.

“Kumekuwa na malalamiko ya polisi kwa baadhi ya madereva wa magari haya katika vituo,tutakuwa tunapima kiwango cha ulevi kwa madereva,tutafunga kamera ambazo zitawezesha RPC au mkuu wa mkoa akiwa hata ofisini kwake anaona yanayoendelea, tumechoka kuona askari wanasingiziwa.

“Tukiambiwa kuna jambo fulani limetokea kituo cha Karatu,saa ngapi na sisi tunaliangalia na tukiona kweli mzee ulivuta kweli pale,tutakuona tu ila kama ulisingiziwa pia tutawaambia,kuna watu walitaka tufunge kamera kwa siri askari wasijue ila tunataka mjue kwa sababu mtakuwa na kazi ya kulinda hizo kamera ,”

Alisema jeshi la polisi kwa kushirikiana na wadau wa utalii wanaweza kuweka utaratibu wa kuyakagua magari hayo walau mara mbili au tatu kwa mwaka na ikiwezekana baadaye watengeneze ‘software’ itakayowezesha kuweka mtandaoni magari ambayo yamekaguliwa hasa kipindi ambacho wageni siyo wengi ‘low season’.

“Heshimuni utaratibu tuliojiwekea nitasikitika ukiwa hauna ufanusi,mimi siyo viongozi wanoona ufahari kumfukuzisha mtu kazi na hata RPC nimemuambua siyo sipati taarifa za maovu yenu, kuna watu wanaoniletea taarifa kama msela wao siyo mkuu wa mkoa ila ukipima unaona ni dogo kuliko mazuri mengi yaliyofanywa,”alisema.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Jonathan Shanna, alisema wataendelea kutoa ushirikiano kwa wadau wa utalii na kuendelea kupunguza changamoto zinazowakabili.

Kuhusu hali ya ulinzi na usalama alisema wataendelea kulinda amani mkoani hapa kwa gharama yoyote.

“Mkoa utakuwa shwari kwa gharama zozote na atakayethubutu zile silaha tulizopewa siyo mapambo zipo vizuri zinafanya kazi zitawashughulikia lakini raia wema tutaendelea kuwalinda,”alisema

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles