25.2 C
Dar es Salaam
Saturday, May 11, 2024

Contact us: [email protected]

Umaskini wa chakula wapungua Tanzania

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Naibu waziri wa fedha, Hamadi Chande  amebainisha  kuwa hali ya umaskini wa chakula imepungua kutokana na Tanzania  kuwa  kiwango kizuri cha upatikanaji  wa chakula.

Amebainisha hayo Novemba 14,2023, jijini Dar es Salaam kwenye kongamano la kujadili masuala mbalimbali yaliyojiri wakati wa utekelezaji wa tafiti zilizofadhiliwa na mradi wa benki ya Dunia uitwao ‘Living Standards Measurement Study-intergrated Survey on Agriculture(LSMS-ISA)’ikiwa pia ni maadhimisho ya miaka 15 ya kufanya utafiti ya hali ya umaskini hapa  nchini na Bara la Afrika.

Amesema programu hiyo ya utafiti iliyoanza 2008 ambayo ilifadhiliwa na benki ya Dunia imeleta msaada mkubwa wa kutambua hali ya upatikanaji wa chakula nchini.

“Kiwango cha umasikini kwa sasa kimepungua hasa umasikini wa upatikanaji wa chakula,chakula kipo kwa wingi cha kutosha ambapo sisi watanzania leo tunalisha mpaka nchi jirani”amesema Chande.

Kwa upande wake mtakwimu mkuu wa serikali Dk. Albina Chuwa, amesema miaka 15 ya utafiti huo umeleta mafanikio makubwa ndani ya Bara la Afrika.

Amesema utafiti huo umefanywa kwa kufuatilia kaya moja moja kwa miaka 15,hivyo 

kupitia utafiti huo umeiwezesha Serikali ya Tanzania na nyingine za Afrika kupunguza umaskini wa chakula.

“Takwimu hizi zimetumika kwenda kwenye program za kuwawezesha watanzania waonyonge hasa maeneo ya vijijini”amesema Dk. Albina.

Amesema wakati utafiti unaanza 2008 katika Bara la Afrika nchi nyingi zilikua zinafanya utafiti kwa kutumia karatasi lakini sasa teknolojia imefanya utafiti unafanywa kwa kutukia vishkwambi.

Naye, Kamisaa wa Sensa, Anna Makinda, amewataka watafiti kurudisha tafiti hizo kwa wananchi kwa maana wao ndio wahusika wakuu.

Amesema utafiti huu umefanikiwa kwa sababu umeweza kumfikia mtu mmoja mmoja na kuelezea ukweli kuhusu maisha yake jambo ambalo si rahisi.

“Hawa wataalam wa takwimu tunasema sasa wakati umefika utafiti wao uenze kuwatumikia hawa wananchi lakini pia utasaidia utendaji wa serikali katika kuwahudumia wananchi wake,”amesema Makinda.

Kwa Upande wake, Chief Economist Afrika Region World Bank, Andrew Dabalen amesema serikali ziwekeze zaidi kwenye utafiti na kuwa na mfuko maalum kwaajili ya utafiti ni muhimu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles